by Admin | 3 September 2024 08:46 pm09
Je ni malaika wawili au mmoja
Swali: Katika Luka 24:4-6, biblia inasema ni malaika wawili..lakini tukirudi katika Marko 16:5-6 tunasoma ni malaika mmoja. Je biblia inajichanganya, au mwandishi yupi yupo sahihi?.
Jibu: Turejee..
Marko 16:5 “Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu”.
Ni kweli hapa biblia inasema ni malaika mmoja, tena ni kijana.
Lakini hebu twende kwenye Luka, tuanzie ule mstari wa 4 hadi wa 6.
Luka 24:4“Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta;
5 nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, HAO WALIWAAMBIA, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?
6 Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya”
Je ni kwamba biblia inajichanganya? Au kuna mwandishi ambaye hayupo sahihi?.
Jibu ni la! Biblia haijichanganyi na wala haijawahi kujichanganya kabisa isipokuwa tafakari zetu ndio zinajichanganya.
Sasa katika maandiko hayo hakuna mwandishi aliyekosea wala anayempiga mwenzake.
Waandishi wote wapo sahihi na malaika waliowatokea ni wanawake wale walikuwa ni wawili na si mmoja.
Isipokuwa malaika aliyesema na wanawake wale ni mmoja kati ya wale wawili na ndiye huyo aliyetajwa na Marko.
Tunajuaje kuwa ni malaika mmoja ndiye aliyekuwa anazungumza na mwingine amenyamaza?.
Tunafahamu kupitia mwandishi wa kitabu cha Luka ule mstari wa 5 unaosema…. “nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, HAO WALIWAAMBIA, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu?….
Hapo anasema “Hao waliwaambia”…sasa kwa kauli hiyo isingewezekana wote waseme kwa pamoja maneno hayo kama maroboti…Ni wazi kuwa ni malaika mmoja ndiye aliyetoa hiyo kauli na hivyo ikawa ni sawa wote wamesema.
Na huyo mmoja aliyetoa hiyo kauli ndiye anayetajwa na Marko…lakini Luka anataja uwepo wa wote wawili.
Ili tuelewe vizuri tutafakari mfano huu… wanahabari wawili wanaripoti hotuba ya Raisi na wa kwanza akasema hivi…. “Raisi wa nchi ya Tanzania amezuia matumizi ya vifungashio vya plastiki”…
Na mwandishi mwingine wa nje aripoti hivi..”Watanzania wazuia matumizi ya vifungashio vya plastiki”.
Je waandishi hawa watakuwa waongo?…au je kuna mmoja atakuwa anampinga mwenzake?..
Jibu ni la! Wote watakuwa sahihi kwani kauli na Raisi ni kauli ya watazania wote…atakalosema Raisi ni sawa na watanzania wote wamesema.
Sawa sawa kabisa na hiyo mwandishi wa Luka…alitaja kauli ya ujumla ya malaika wote wawili na Marko akataja ya mmoja tu (yule aliyetoa kauli).
Je umempokea Bwana YESU KRISTO?.
Kama bado unasubiri nini?..ule mwisho umekaribia sana na Bwana YESU amekaribia kurudi sana.
Ikiwa utahitaji msaada wa kumpokea Bwana YESU basi waweza wasiliana nasi na tutakuongoza sala ya kumkiri Bwana YESU baada ya wewe kumwamini.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
Biblia inaposema Yesu ameketi mkono wa kuume inamaana gani?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/09/03/je-ni-malaika-wawili-au-mmoja/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.