VITOE VIUNGO VYAKO VITUMIKE KWA HAKI UPATE KUTAKASWA.

by Admin | 22 September 2024 08:46 pm09

Je unajua UTAKASO hauji tu kufumba na kufumbua????…


Nguvu ya utakaso (yaani Roho Mtakatifu) unaweza kuipokea kufumba na kufumbua, lakini mpaka ule mzizi wa dhambi uondoke ndani yako inachukua muda kidogo (inahitaji juhudi).

Ulikuwa ni mzinzi, siku umepokea ujazo wa Roho sio mwisho wa vita, 

Sasa ili upokee utakaso mkamilifu, utakaoondoa mzizi wa dhambi kama usherati, kujichua, kuua, kuiba, kusengenya n.k ni lazima uvitoe viungo vyako vitumike katika haki.

Maana yake ule mdomo uliokuwa unautumia kusengenya sasa utumie kuhubiri, ule ulimi uliokuwa unautumia kutukana sasa unaanza kujizoeza kuutumia kuomba..

Kile kinywa kilichokuwa kinatumika kuimba nyimbo za kidunia, sasa unautumia kumwimbia Mungu sifa.

Yale macho yako uliyokuwa unayatumia kutazama picha za tupu mitandaoni, na kusoma makala za uzinzi… sasa unayatumia kusoma Neno la Mungu.

Ule mwili wako ulikuwa unauchosha kwa ulevi sasa unabadilisha matumizi kwa kuanza kufunga na kuomba.

Kama ulikuwa unafanya uzinzi na ukahaba sasa unautumia mwili wako kuhubiri injili nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa..

Kwa kufanya hivyo, UTAKASO utaingia ndani yako. Kwasababu sasa VIUNGO vyako unavitumia kufanya haki…ndivyo biblia inavyotufundisha..

Warumi 6:19 “Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa”. 

Umeona??..kwa kuvitoa viungo vyako vitumiwe na Haki unapata UTAKASO…Maana yake ule uzinzi uliokuwa unaona ni mgumu kuuacha, utaona umeondoka ndani yako.

Ule usengenyaji uliokuwa unaona ni mgumu kuacha, utaona unapotea ndani yako na tabia nyingine zote ni hivyo hivyo…

Lakini kama ukipokea Roho Mtakatifu halafu viungo vyako huvizoezi  kufanya haki, ni ngumu kutakasika!!!!…utapambana na uasherati miaka na miaka hutauacha, utapambana na ulevi miaka na miaka, hutaona badiliko lolote, hata kama  ulibatizwa ubatizo ulio sahihi, na kujazwa Roho siku ile…bado hutaona badiliko lolote.

Jizoeze kuomba (bila kushurutishwa) ndugu uliyempokea Kristo, jizoeze kuhubiri ndugu, jizoeze kumwimbia Mungu, jizoeze kusoma Neno, jizoeze kuutumia mwili wako kufanya mambo yote ya kiungu na utaupokea utakaso (hiyo ni Biblia).

Warumi 6:22 “Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KIJITO CHA UTAKASO.

ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.

KILA KIUNGO LAZIMA KISHUGHULIKE.

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

JE UNAZAA MATUNDA NA KUWAPONYA MATAIFA?

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/09/22/vitoe-viungo-vyako-vitumike-kwa-haki-upate-kutakaswa/