ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.

ZIDI KUTAFUTA UTAKASO WA MWILI.

Shalom.

Usiishie kutafuta tu utakaso wa roho, bali tafuta pia UTAKASO WA MWILI, kwamaana vitu hivi viwili vinaenda sambamba, kwasababu vitu hivi vikichafuka vinaiharibu pia nafsi ya mtu.

2Wakorintho 7:1“Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na UCHAFU WOTE WA MWILI NA ROHO, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”.

Upo usemi kuwa Mungu wetu hatazami sana Mwili, lakini anatazama Zaidi Roho ya Mtu. (Hatuna budi kuwa makini na kauli hii!!)

Kutokana na kwamba asilimia kubwa ya maombi yetu yanalenga MAHITAJI YA MWILINI, basi ni wazi kuwa Mungu anaitazama pia miili yetu. Kwasababu kama mtu atamwomba Mungu Baba ampe fedha, au chakula, au makazi hayo yote si kwasababu ya “roho” kwasababu roho haili chakula, wala haivai nguo, wala haiishi kwa fedha.. bali mwili ndio unaohitaji hayo yote.

Sasa kama tutamlazimisha Mungu Baba aangalie miili yetu kwa mahitaji yetu, halafu wakati huo huo tunasema Mungu haangalii mwili, tutakuwa WANAFIKI!!.

Sasa ikiwa asilimia Zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yetu, yanalenga MIILI YETU, Basi ni wazi kuwa Mungu anaangalia Miili yetu na anajishughulisha nayo sana….

Ni lazima kulijua hili ili tusipotee na elimu ya uongo ya shetani,.. Ni lazima pia tujishughulishe kutafakari namna ya kuyafanya mapenzi ya Mungu katika miili yetu kama tu vile tunavyojishughulisha katika kumwomba mahitaji ya mwili..

1Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; NANYI NAFSI ZENU NA ROHO ZENU NA MIILI YENU mhifadhiwe MWE KAMILI, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo”.

Katika mstari huo biblia imetaja mambo yote matatu; Nafsi, mwili na roho. (yanapaswa yawe makamilifu, bila lawama mpaka wakati wa kuja kwake Bwana YESU).

Hivyo zingatia yafuatayo:

  1. NI NINI UNAFANYA KUPITIA MWILI WAKO.

Jipime ni nini unakifanya katika mwili,.. je shughuli au matendo unayoyafanya kupitia mwili wako ni kulingana na mapenzi ya Mungu??.. Kama unafanya kazi haramu (mfano ukahaba, au kazi ya kuuza vitu haramu kama pombe, sigara, na mengineyo), basi kazi hiyo unaifanya kupitia mwili wako hivyo ibadili ili isikupeleke jehanamu ya moto.

Kama matendo unayoyafanya katika mwili ni  haramu mfano uzinzi (1Wakorintho 6:18), wizi, au mauaji n.k geuka leo yasije yakawa sababu ya kukupeleka hukumuni.

   2. NINI UNAKIAMBATANISHA NA MWILI WAKO

Angalia ni nini unakiambatanisha/unakishikamanisha na mwili wako.. Hapa nazungumzia aina ya mavazi na urembo na michoro (tattoo). Je mavazi uvaayo ni sawasawa na Neno la Mungu?.. Je yanaipasa jinsia yako sawasawa na Kumbukumbu 22:5.

Je mavazi unayovaa ni ya kujisitiri?, kuzuia tamaa kwa upande mwingine na kutunza heshima yako? (1Timotheo 2:9 na Mathayo 5:28)

Je michoro uichorayo na rangi yako ya asili uiondoayo ni mapenzi ya Mungu? (Walawi 19:28)

Angalia ni nini kinanin’ginia mwilini mwako.. Je hizo cheni, hereni, mikufu, bangili, vikuku n.k ni mapenzi ya Mungu?? Je si ishara ya utumwa?? (hebu soma Kutoka 21:5-6 na Kumbukumbu 15:16-17).

   3. NI NINI KINAINGIA MWILINI MWAKO.

Angalia ni kitu gani unakiingiza mwilini mwako.. Je Mungu amekusudia moshi uingia katika mapafu yako ambayo yanapaswa yavute hewa safi ili kutimiza miaka uliyopewa yakuishi duniani?..

Je Mungu amekusudia uingize vilevi na madawa ya kulevya ndani ya mwili wako na kukutoa ufahamu wako kwa muda?.. Jiulize kama si ruhusu kuendesha chombo chochote cha moto ukiwa umelewa/umekunywa pombe.. vipi kuuendesha huo mwili ukiwa umelewa??.. Huoni kama huo ni uvunjaji wa sheria kubwa Zaidi, kwasababu mwili ni bora kuliko gari au chombo kingine chochote cha usafiri.

2Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.

KIJITO CHA UTAKASO.

Nini Maana ya Adamu?

WEWE SI MALI YAKO MWENYEWE!

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments