Kwanini Bwana MUNGU aliwazuia Adamu na Hawa wasile matunda ya Mti wa uzima waishi milele?

by Admin | 3 October 2024 08:46 am10

Swali: Kulikuwa na ubaya gani wa Adamu na Hawa kula matunda ya mti wa Uzima, ili wapate tena uzima wa milele baada ya kuupoteza? (Mwanzo 3:22-24).


Jibu: Turejee mistari hiyo..

Mwanzo 3:22 “Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, AKALA, AKAISHI MILELE;

23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa”.

Sababu pekee ya Bwana MUNGU kuwazuia wazazi wetu wa kwanza (Adamu na Hawa) kula yale matunda ya Mti wa Uzima, si kwamba Mungu alikuwa hataki waishi milele!. La!.. kinyume chake ni mpango wake mkamilifu wa Mungu kwamba mwadamu aishi milele.

Tito 1:2 “katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema uongo aliuahidi tangu milele”

Soma pia 1Yohana 2:25 utaona jambo hilo hilo…

Lakini kwasababu tayari mwanadamu alikuwa ameshaiingiza dhambi ndani yake na katika kizazi chake, hivyo asingeweza kuishi milele katika dhambi, hivyo ni lazima dhambi iondoke kwanza ndani yake ndipo aishi milele, kwasababu kama akiishi milele na dhambi imetawala maisha yao, ni uharibifu mkubwa utaendelea na maisha yatakuwa nje na mpango wa Mungu, kwasababu yeye Mungu ni mkamilifu, hivyo kanuni ya maisha ya milele, ni sharti yasiwe na dhambi.

Kwahiyo BWANA MUNGU akaweka mpango kwanza wa kuiondoa dhambi ndani ya mtu, na mzizi wake, kisha yule mtu apate tena uzima wa milele.

Na mpango wa Mungu wa kuondoa dhambi ndani ya Mtu na kumrejeshea Uzima wa milele, ameushona ndani ya Mwanae YESU KRISTO, kwamba kwa kupitia njia ya kumwamini yeye, na kutubu basi tunaoshwa dhambi zetu na kupata uzima wa milele.

Warumi 5:21 “ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu”.

17  Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”.

Hivyo kamwe hatuwezi kupata uzima wa milele, tukiwa katika dhambi..ni lazima kutubu kwanza na kumwamini Bwana YESU ndipo tupate uzima wa milele.

Na hiyo ndio sababu ya Bwana MUNGU kuifunga ile njia ya MTI WA UZIMA pale Edeni, ilikuwa ni sharti kwanza ADAMU na HAWA watakaswe ndambi zao kwa damu ya Mwanakondoo… Na majira yalipofika Mungu alimtuma mwanae ili afe kwaajili ya wote walio hai, na waliokwisha kutangulia, waliokufa katika haki, ili kwamba wote tutakaswe na kupata uzima wa milele.

Na hili ni la kujua siku zote, kwamba hakuna uzima wa milele kwa mwingine yeyote Zaidi ya YESU KRISTO.

Yohana 3:35 “Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake.

36  Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia”.

Mistari ifuatayo inazungumzia uzima wa milele ndani ya YESU KRISTO (1Yohana 5:11-13, Yohana 3:16, Yohana 5:24,  Yohana 6:54,  Yohana 12:50, Yohana 17:2, na Warumi 6:23)  .

Je umempokea BWANA YESU?… kama bado unangoja nini?..Fahamu kuwa hizi ni siku za mwisho, majira yameenda sana na ule mwisho umekaribia.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NAO WALIOKUWA WAMEKUSUDIWA UZIMA WA MILELE WAKAAMINI.

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

INJILI YA MILELE NI IPI KATIKA BIBLIA?

MJUE SANA YESU KRISTO.

NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/10/03/kwanini-bwana-mungu-aliwazuia-adamu-na-hawa-wasile-matunda-ya-mti-wa-uzima-waishi-milele/