by Admin | 8 November 2024 08:46 am11
SWALI: Shuleni tumefundishwa sayari zipi Tisa Lakini je maandiko yanasemaje kuhusu hili, je zipo kweli kwa idadi hiyo?
JIBU: Biblia si kitabu cha kisayansi, au cha taaluma yoyote, kwasababu lengo lake sio uvumbuzi na utafiti wa mambo ya ulimwenguni. Bali ni kumrejesha mwanadamu kwa muumba wake. Ni kitabu chenye msingi wa IMANI. Mambo yasiyothibitika kwa macho bali rohoni. Ni kitabu kielezacho njia ya ukombozi wa mwanadamu inayopatikana kupitia YESU KRISTO mwokozi wa ulimwengu.
Ijapokuwa vipo vifungu vichache vichache vinavyoelezea uhalisia wa elimu za duniani, lakini isidhaniwe kuwa lengo lake kuu ni kutoa taarifa za kila kitu kwenye hii dunia, bali mara nyingi huwa ni kuelezea vema habari husika ya rohoni iliyokuwa inazungumziwa hapo.
Tukirudi kwenye swali linalouliza kuhusu sayari, kwamba sayansi inatuambia zipo tisa, je biblia nayo inazitaja ngapi?
Kama tulivyotangulia kusema biblia haielezi kila kitu kuhusu dunia hii, bali inaeleza kila kitu kuhusu wajibu wa mwanadamu kwa muumba wake.
kuhusu Sayari biblia inazitaja bila shaka kwamba yeye ndio aliziumba, na magimba yote angali, ambayo yamejumuishwa katika neno jeshi la mbinguni .
Katika biblia sayari zimejatwa kwenye vifungu hivi;
Ayubu 38:32
[32]Je! Waweza kuziongoza Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
2 Wafalme 23:5
[5]Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni.
Lakini biblia Haijatoa idadi, kama ni tisa, au mia au elfu Mungu alizoziumba, bila shaka ni nyingi, kwani turudipo kwenye sayansi, ndio tunathibitisha kuwa zipo mabilioni kwa mabilioni kwa mabilioni, hizi tisa walizoziona ni ambazo zipo tu kwenye mfumo wa jua letu..lakini huko angani kuna ma-jua mengi yasiyo hesabika na yote hayo yana sayari zake. Hata hivyo husema hizi nyota zote tuzionazo angani ni ma-jua kama hili letu isipokuwa tu yapo mbali sana.
Kwahiyo wanasayansi hututhbitishia zaidi uweza wa ajabu wa Mungu. Mambo yasiyoelezeka kwa ukuu na maarifa. Utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Lakini Je! umempokea huyu Mungu aliyeumba mambo haya ya ajabu? kumbuka kumpokea yeye ni kumwamini Yesu. Kuaminije? . Ni kuamini ile kwa ile kazi yake kamilifu ya ukombozi wetu aliyotutenda sisi kwa kifo chake pale msalabani, iletao ondoleo la dhambi.
Ikiwa upo tayari leo kumpokea huyu mwokozi basi bofya hapa kwa mwongozo wa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Je! dunia Ni duara, tufe au ipo kama sahani?biblia inasemaje?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/11/08/biblia-inasema-nini-kuhusu-sayari-je-ni-kweli-zipo-tisa/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.