Jeshi la Mbinguni wana wa Israeli waliloliabudu ni lipi?

Jeshi la Mbinguni wana wa Israeli waliloliabudu ni lipi?

SWALI: Ni jeshi gani la Mbinguni ambalo Mungu aliwaacha wana wa Israeli waliabudu katika Matendo 7:42? Je ni Malaika au?


JIBU: Matendo 7: 41  “Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. 

42  Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?”

Habari hii inawazungumzia wana wa Israeli wakati wanatoka Misri. Wakiwa jangwani biblia inasema walikuwa wakikengeuka mara kadhaa, walikuwa wakimwacha Mungu na kugeukia kuchonga sanamu, na wakati mwingine kumjaribu Mungu (Kutoka 17:2).

Lakini kuna jambo lingine tunaliona walilokuwa wanalifanya ambalo lilikuwa ni machukizo kwa Mungu, na hilo si lingine zaidi ya KULIABUDU JESHI LA MBINGUNI.

Sasa swali la msingi hapo ni je! Hilo jeshi ni lipi?, ni malaika au ni nini?.

Jibu ni kwamba si Malaika, bali ni miungu ya kipagani. 

Si kila mahali kwenye biblia palipoandikwa neno “mungu” panamaanisha “Mungu wa mbingu na nchi”, vivyo hivyo sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “bwana” panamaanisha “Bwana Mungu wa mbingu na nchi”…hali kadhalika sio kila mahali katika biblia palipoandikwa neno “mbingu” au “mbinguni”, panamaanisha “Mbinguni malaika watakatifu walipo”..

Dini karibia zote zinaamini kwamba kuna mbingu..kwamba kuna mahali huko juu ambapo kuna viumbe watakatifu wanaishi,..Na nyingine zinaamini huko mbinguni kuna miungu mingi, kuna jeshi kubwa la miungu, ambayo yote inastahili kuabudiwa. Kwamfano dini ya kihindu tu peke yake ina zaidi ya miungu milioni 330. 

Sasa ikatokea kwa mtu ambaye ni mkristo, ambaye ameshajua ukweli wote kwamba Mungu ni mmoja tu aliyeko mbinguni ambaye anaabudiwa katika roho na kweli.. akaiacha hiyo imani na kisha akaenda kujiunga na imani nyingine(kama hiyo ya kihundu) inayoamini kwamba mbinguni kuna miungu mingi, na akaenda kuiabudu hiyo miungu yao. Hapo ni sawa na kusema “AMEKWENDA KULİSUJUDİA JESHİ LA MBİNGUNİ”..na si mbingu ile ambayo malaika watakatifu wapo bali ni mbingu ya kihindu, ambayo kiuhalisia haipo! ni uongo uliotengenezwa na shetani tu kuwadanganya watu kuwa kuna mbingu yenye miungu mingi!,

Ni agenda ya  shetani na mapepo yake Kutafuta kuabudiwa na kuwapotosha watu wa Mungu. Hiyo idadi yote ya miungu wanayoiabudu ni mapepo yanayojiguza na kuchukua sura ya hivyo wanavyoviabudu. (zingatia: wengi wanaoabudu hiyo miungu, sio watu wabaya na wala si maadui zetu, wengi wao ni watu wazuri, wanafanya hayo kwasababu bado hawajaujua ukweli, au macho ya mioyo yao bado hayajafumbuliwa, kwahiyo wanaabudu vitu wasivyovijua, hivyo ni jukumu letu wewe na mimi kuwapelekea injili na kuwaombea!, ili macho yao yafumbuliwe wapate kuona na kuokolewa Matendo 17:29-31).

Kwahiyo Jeshi la mbinguni linalozungumziwa hapo sio Malaika waliopo mbinguni, bali ni miungu  iliyopo mbinguni huko angani, ambayo kiuhalisia ni shetani na mapepo yake.

Na malkia wa mbinguni aliyezungumziwa pia katika Yeremia 7:18, 44:17-25 sio Bikira Mariamu wala sio Malaika fulani wa kike aliyeko mbinguni bali ni mungu fulani wa kipagani, wanayedai kwamba yupo mbinguni (kwa maelezo marefu utatutumia ujumbe inbox), ambaye ni Pepo!.

Mwisho ni muhimu kuchukua tahadhari!.. pale tunapoonywa mara nyingi!…Hapo kwenye matendo 7:42, biblia inasema “ Basi MUNGU AKAGHAİRİ, AKAWAACHA ili waliabudu jeshi la mbinguni,”. 

Litazame hilo neno kwa makini!..Mungu akaghairi!, akawaacha!! İli waliabudu jeshi la mbinguni…Ni jambo la kuogopesha sana pale Mungu anapoghairi juu yako, na kukuacha uendelee kufanya unayoyafanya!…hilo ni jambo la kuogopesha sana!..Anaabudu masanamu unayodhani ni watakatifu Fulani wa mbinguni, na umeonywa mara nyingi husikii, hapo unamfanya Mungu aghairi juu yako.

Warumi 1:28  “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa”

 

2Wathesalonike 2:10  “na katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo”.

Jiupeshe na ibada za sanamu ni dhambi, jiepushe na mambo yote maovu na mwisho soma neno kwa bidii..

Bwana atubariki.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.

AINA YA MAADUI UTAKAOKUTANA NAO KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments