Je kuna pepo wazuri kulingana na Waefeso 6:12?

by Admin | 13 December 2024 08:46 am12

Swali: Biblia inasema kushindana kwetu ni dhidi wa pepo wachafu, je kulingana na mstari huo, wapo pepo wazuri?


Jibu: Turejee…

Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya MAJESHI YA PEPO WABAYA katika ulimwengu wa roho”

Biblia iliposema kuwa kushindana kwetu ni dhidi ya “pepo wabaya” haijamaanisha kuwa wapo pepo wazuri, bali inaelezea tu sifa ya hizo roho (mapepo) kwamba ni mbaya na chafu.

Ni sawa na biblia inapotaja Malaika watakatifu, (soma Mathayo 25:31, Marko 8:38 na Ufunuo 14:10) haimaanishi kuwa wapo Malaika wasio watakatifu, na kama wapo wasio watakatifu basi hawaitwi tena Malaika bali ni mapepo, vile vile hakuna mapepo wasafi na kama zipo hizo roho safi basi haziwezi kuitwa tena mapepo, bali zitaitwa Malaika.

Hivyo uzuri na usafi unaotajwa juu ya Malaika au Mapepo, ni kuelezea tu sifa zao na kazi zao, kwamba Malaika wote walioko mbinguni ni wasafi na watakatifu, na mapepo yote yaliyotupwa ulimwenguni ni machafu na mabaya.

Na kumbuka pia “Pepo na jini” ni kitu kimoja, isipokuwa ni lugha mbili tofuati tu!… Na hakuna jini wala pepo mzuri, wote ni wabaya na wachafu. Zipo dini zinazofundisha kuwa wapo majini (mapepo) wazuri, na kwamba watu wanaweza kuwa nao na wakawaletea mafanikio na hata kuwalinda.

Huo ni uongo wa shetani asilimia mia, kwani shetani ndiye baba wa uongo..

Yohana 8:44 “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; KWA SABABU YEYE NI MWONGO, NA BABA WA HUO”.

Shetani hajawahi kuwa na urafiki wa kweli na mwanadamu, wala hajawahi kuwa na mapenzi na mwanadamu, kitu anachokipenda kutoka kwa mwanadamu ni utukufu tu!.. lakini hajawahi kumpenda mwanadamu, na hakuna unabii ya kwamba atakuja siku moja kumpenda mwanadamu, yeye ni adui wa mwanadamu wa milele.

Na Kama tu shetani asivyopendwa kuitwa shetani, bali anapendwa aitwe mungu, kadhalika hawezi kuruhusu mapepo yake yaitwe vibaya, kwa sifa mbaya?..atawakatakasa tu!.. na anawatakasaje?..si kwa njia nyingine bali kwa njia za dini za uongo, zinazohubiri na kufundisha kuwa wapo mapepo wazuri.

Kwa urefu kuhusiana na pepo wachafu(majini) fungua hapa >>

MAJINI WAZURI WAPO?

Je umempokea YESU?.. kama bado ni nini kinakungojesha?

Bwana anarudi.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Rudi Nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2024/12/13/je-kuna-pepo-wazuri-kulingana-na-waefeso-612/