by Admin | 2 January 2025 08:46 am01
Swali: Je shetani yule audanganyaye ulimwengu alitoka wapi?
Jibu: shetani kwa asili aliumbwa na Mungu, na kabla ya kuwa shetani alikuwa akiitwa “Kerubi afunikaye”
Ezekieli 28:14 ” Wewe ulikuwa KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA AFUNIKAYE; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto”.
Na MUNGU alimwumba akiwa mkamilifu (asiye na dosari) kama tu MAKERUBI wengine, lakini baadaye moyo wake uliinuka akajidanganya mwenyewe kuwa anaweza kuwa kama MUNGU (aabudiwe kama MUNGU) Na ndipo Uovu huo ukaonekana ndani yake, na hakutaka kubadilika.
Ezekieli 28:15 “Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako”
Na baadaye alipoasi ndipo akawa shetani, na maana ya shetani ni Mshitaki/Mchongezi, maana yake anawashitaki wanadamu mbele za MUNGU mchana na usiku.
Ufunuo 12:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana AMETUPWA CHINI MSHITAKI WA NDUGU ZETU, YEYE AWASHITAKIYE MBELE ZA MUNGU WETU, MCHANA NA USIKU”.
Kwahiyo shetani aliumbwa na MUNGU, na akaasi na ataharibiwa na MUNGU katika ziwa la MOTO baada ya hukumu ya kile kiti cheupe.
Ufunuo 20:10 “Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele”.
Bwana atuepushe na ibilisi.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/01/02/shetani-alitoka-wapi/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.