by Admin | 13 January 2025 08:46 pm01
Jibu: Turejee.
Isaya 1:31 “Na mtu hodari atakuwa kama MAKUMBI, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima”.
“Makumbi” ni malighafi yoyote inayotumika katika kuanza au kuchochea moto, mfano; mbao, vijiti au nyasi kavu.
Katika kitabu hiko cha Isaya, biblia imemtaja mtu hodari kwamba siku hizo atakuwa si kitu bali kama tu vijiti vishikavyo moto na kuteketea.
Isaya 1:28 “Lakini kuharibika kwao wakosao nao wenye dhambi kutatokea wakati mmoja, nao wamwachao Bwana watateketezwa.
29 Kwa maana watatahayarika kwa sababu ya mialoni mliyoitamani, nanyi mtaaibishwa kwa sababu ya bustani mlizozichagua.
30 Maana mtakuwa kama mwaloni ambao majani yake yakauka, na kama bustani isiyo na maji.
31 Na mtu hodari ATAKUWA KAMA MAKUMBI, na kazi yake kama cheche ya moto; nao watawaka pamoja, wala hapana atakayewazima”.
Bwana hata sasa atusaidie tusimwache, bali tuzishike amri zake na maagizo yake ili tusiteketee kwa moto wake.
Yeremia 5:11 “Maana nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamenitenda kwa hiana sana, asema Bwana.
12 Wamemkataa Bwana, na kusema, Si yeye; wala hayatatupata mabaya; wala hatutaona upanga wala njaa;
13 na manabii watakuwa upepo, wala neno lake halimo ndani yao; basi ndivyo watakavyotendwa.
14 Kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa majeshi, asema hivi, Kwa sababu mnasema neno hili, tazama, nitafanya maneno yangu katika KINYWA CHAKO KUWA MOTO, NA WATU HAWA KUWA KUNI, NAO MOTO UTAWALA”
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/01/13/makumbi-ni-nini-isaya-131/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.