Na si miaka yake tu ambayo haijatajwa bali hata kabila lake Mariamu, wala ukoo wake….Na kwanini biblia haijarekodi mambo hayo yamhusuyo Maramu?….Jibu: Ni kwasababu si wa muhimu sana sisi kuujua…
Tunachojua ni kuwa Mariamua alikuwa ameshafikia umri wa kutosha wa kujitambua ndio maana tayari alikuwa ametolewa posa.. Hivyo alikuwa na umri wa kutosha na alikuwa mnyenyekevu na aliyemcha MUNGU.
Umri wa Mariamu, au familia aliyotokea au kabila alilotokea havikuwa vya umuhimu sana sisi kuvijua, kwasababu Mariamu alikuwa ni mwanamke tu kama wanawake wengine, alipata tu neema ya kumzaa Bwana YESU lakini hakuwa na utofauti na wanawake wengine waliomcha MUNGU.
Kwahiyo kilichokuwa cha muhimu sana sisi kujua ni kwamba “bikira atachukua mimba”…sawasawa na unabii wa Isaya.
Isaya 7:14 “Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli”.
Na hapo hasemi… “ bikira atachukia mimba akiwa na miaka 20 au 25 au 30”.. La! haisemi hivyo.. ikimaanisha kuwa lililo la msingi kwetu kulifahamu ni hilo la bikira kuchukua mimba basi, hayo mengine hayana umuhimu hivyo yanabaki kuwa ya Mungu na ya wale waliokuwepo wakati Mariamu anachukua ujauzito..
Kumbukumbu 29:29 “Mambo ya siri ni ya BWANA, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii”.
Wapo wanaomwona Mariamu kama mwanamke aliye tofauti na wanawake wengine wote, kwamba anaweza kusimama katika nafasi ya kutuombea au hata kutubariki, na hivyo anapaswa apewe heshima ya kipekee, na hata inaaminika pia kwa baadhi ya watu kuwa alipaa, jambo ambalo pia ni uongo.
Dhana ya kuwaamini manabii na watu waliopokea neema kwenye biblia kuwa ni watu wakuu sana wa kusimama katika nafasi ya kuombwa au kutukuzwa ilianza tangu zamani kabla hata ya ujio wa Bwana YESU.
Wapo waliokuwa wanamwabudu Henoko aliyetwaliwa, wapo waliokuwa wanamwabu Musa, wengine Eliya wengine Daudi, na sasa wapo wanamwabudu Mariamu n.k, lakini hawa wote biblia inasema ni watu kama sisi tu..
Yakobo 5:17 “Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita”.
Sasa kama Eliya aliyepaa mbinguni biblia inasema alikuwa ni mtu kama sisi vipi hao wengine ambao walikufa??…
Ambaye hakuwa mtu wa kawaida ni Bwana YESU tu na huyo ndiye maandiko yanasema anastahili kuabudiwa kwa kuwa alimwaga damu yake kwaajili yetu..
Ufunuo wa Yohana 5:8 “Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa”.
Je umempokea Bwana YESU…Umebatizwa katika ubatizo sahihi?.
Kama bado basi fanya uamuzi leo, kwasababu hizi ni siku za mwisho na YESU yupo mlangoni.
Bwana akubariki.