Tunathibitisha vipi kuwa Yule Malaika wa (Yohana 5:4) ni wa MUNGU?

by Admin | 17 April 2025 08:46 am04

Swali: Je! tunaweza kuthibitisha vipi kuwa Yule malaika aliyekuwa anashuka na kuyatibua maji alikuwa ni malaika wa MUNGU na si wa shetani, kwasababu maandiko yanasema  kuwa shetani naye anaweza kujigeuza na kuwa mfano wa malaika wa nuru (2Wakorintho 11:14).

JIbu: Turejee..

Yohana 5:1 “Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu. 2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.

3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.

4 Kwa maana kuna wakati ambapo MALAIKA HUSHUKA, AKAINGIA KATIKA ILE BIRIKA, AKAYATIBUA MAJI. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, AKAPONA UGONJWA WOTE ULIOKUWA UMEMPATA.]”

Ni kweli Biblia inasema shetani anaweza kujigeuza na kuwa mfano wa Malaika wa Nuru, lakini haisemi kuwa anaweza kujigeuza na kuwa Malaika wa Nuru, bali mfano wa..

Kwahiyo huyu tunayemsoma hapa katika Yohana 5:4 hakuwa malaika wa giza, kwasababu matunda yake si ya giza kwani Maandiko yanasema “shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake”.

Mathayo 12:25 “Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama.

26 Na SHETANI AKIMTOA SHETANI, AMEFITINIKA JUU YA NAFSI YAKE; basi ufalme wake utasimamaje?”

Sasa wote waliokuwa wamelala pale walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa yaliyoletwa na mapepo, kwasababu asilimia kubwa ya magonjwa yanasababishwa na mapepo (soma Mathayo 9:32 na Mathayo 12:22).

Sasa kwa mantiki hiyo haiwezekani malaika wa giza kushuka na kuwatoa malaika wenzake wa giza (yaani mapepo) wenzao ndani ya watu, ni jambo ambalo haliwezekani!, vinginevyo ufalme wa giza usingesimama, kwahiyo Yule malaika alikuwa anashuka kuyatibua maji ni malaika wa Nuru na si wa giza.

Jambo la ziada la kujifunza ni kwamba watu wanaokwenda kwa waganga wa kienyeji kwaajili ya kutatuliwa shida zao au magonjwa yao na baada ya kupiga ramli wanaona kama wamepona..

 Kiuhalisia ni kwamba hawajatatuliwa matatizo yao bali ndio yameongezwa, kwamfano mtu ataenda kwa mganga akiwa na tatizo la homa, na anaaguliwa na kujiona amepona kabisa, na kuambiwa kuwa majini yamefukuzwa ndani yake.

Sasa kiuhalisia kulingana na biblia yale mapepo hayajaondoka!, bali yamehamishwa kutoka sehemu moja ya mwili kwenda nyingine, au kutoka sehemu moja ya maisha kwenda nyingine, lakini si kwamba yamefukuzwa/kuondolewa kabisa kutoka katika maisha yake,

 Maana yake sasa huyu mtu atapata unafuu kwenye kifua kilichokuwa kinamshumbua, au kwenye mguu, lakini lile pepo limehamia kwenye tumbo, au miguu, au limepelekwa kusababisha matatizo mengine katika maisha ya Yule mtu, na tena mtu anayeenda kwa mganga anakuwa anaongezewa mapepo mengine kwa ajili ya matatizo mengine yatakayotokea wakati huo huo au wakati mwingine huko mbeleni, kwasababu shetani kamwe hawezi kumtoa shetani mwenzake.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

BIRIKA LA SILOAMU.

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

JE BADO UNASUBIRIA MAJI YACHEMKE?

AKAWAPONYA WALE WENYE HAJA YA KUPONYWA

WAKO WATATU WASHUHUDIAO MBINGUNI NA DUNIANI.

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/04/17/tunathibitisha-vipi-kuwa-yule-malaika-wa-yohana-54-ni-wa-mungu/