by Devis | 31 May 2025 08:46 am05
Dini ni mfumo au utaratibu wa kumwabudu Mungu. Kwamfano ukienda mahali ukaona watu wamekusanyika na kukubaliana kuabudu kitu Fulani, ni lazima utaona tu utaratibu, au mwongozo au miiko wamejiwekea ya kuifuata na kuishika, ili ibada yao iwe na matokeo. Sasa huo utaratibu ndio unaitwa dini.
Hata imani yetu ndani ya Kristo, inasukumwa na dini. Hatumwabudu tu Mungu kama tunavyotaka bali Mungu aliweka utaratibu na njia ya kuifuata.
Lakini Dhehebu, ni “aina ya dini”. Ambayo huzalika ndani ya imani ile ile moja. Kwamfano utaona wakristo imani yao ni moja kwa Kristo Yesu, na msingi wa kuegemea ni biblia ile ile moja takatifu. Lakini ndani yao kuna michipuko mingi tofauti tofauti ya kitaratibu na ufanyaji ibada, kulingana na walivyoielewa biblia. Ndio hapo utaona wengine wanajiita wapentekesto, wengine wakatoliki, wengine wasabato, n.k. Sasa hii yote ni michupuko, ambayo mengine inakaribiana sana na uhalisia, na mengine inakwenda mbali na kweli ya Mungu.
Lakini cha kumshukuru Mungu ni kuwa biblia imeshaeleza asili ya dini ya kweli inapaswa iweje….
Yakobo 1:26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. 27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Kwamba ni lazima itakuwa ya kimatendo zaidi. Yaani utafunzwa utakatifu, na kujitoa.
Hapana, kwasababu Yesu hakuja kuleta dhehebu jipya duniani. Kwani alipokuja alikuta tayari yapo madhehebu mengi yamesha-zaliwa kama tu ilivyo sasa, mfano Mafarisayo, na masadukayo. Lakini hakuwahi kutetea lolote kati yao. Bali alisisitiza watu kumwamini yeye, kama ndio njia ya kweli na uzima mtu asipofanya hivyo hawezi kumwona Baba (Yohana 14:6).
Ikiwa na maana haijalishi una dhehebu zuri kiasi gani. Ukikosa shabaha ya Ukristo, bado mbinguni huendi. Waamini wengi wanashikilia zaidi dini, jambo ambalo ni jema, lakini dini ni kisaidizi cha imani. Sio imani yenyewe, ni sawa na shule na elimu, tunaweza kusema shule ni kisaidizi cha elimu, lakini sio elimu yenyewe.
Hivyo ni busara kuchukua tahadhari ya dhehebu unalotaka kumwabudia Mungu, kwasababu ukweli ni kwamba madhehebu mengine hayana ubora wa kumfanya mtu awe mkristo kamili.
Kwamfano dhehebu lisilo, patana na imani katika Kristo Yesu tu, au lisilofundisha utakatifu, au lisilo amini juu ya vipawa vya Roho Mtakatifu, au linalochanganya ibada ya Mungu na sanamu, bali linasisitiza mambo ya mwilini tu, hilo halikujengi, bali linakupoteza.
Lifananishe kwanza na biblia yako, huku ukimwomba Roho Mtakatifu akusaidie, kisha ndio ufanye maamuzi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Kwanini kuna tafsiri nyingi za Biblia, na tafsiri ipi ni sahihi?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/05/31/tofauti-kati-ya-dhehebu-na-dini-ni-ipi/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.