JE NI YESU YUPI UNAYE? WA KIDINI AU WA UFUNUO!

JE NI YESU YUPI UNAYE? WA KIDINI AU WA UFUNUO!

Jina la Bwana na Mwokozi Mkuu YESU KRSTO libarikiwe daima!

Kuna tofauti ya kumjua YESU WA KIDINI na yule wa UFUNUO (Yaani Yesu aliyefunuliwa maishani mwako na yule uliyempokea kwa wazazi au kwa mhubiri fulani)  Utauliza kivipi?..Hebu tumwangalie mtu mmoja katika biblia ambaye hapo kwanza alimjua YESU wa kidini lakini baadaye akaja kumpokea wa KIUFUNUO, Na ikawa heri kwake!. Na mtu huyo si mwingine Zaidi ya Petro.

  1. YESU WA KIDINI.

Yohana 1:40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

41  Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, TUMEMWONA MASIHI (MAANA YAKE, KRISTO).

42  Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe)”

Hapa Petro anamjua  na kumpokea YESU kwa kuambiwa TU!!!…Anaambiwa na Adrea kaka yake habari za YESU, hivyo Petro anaamini na akampokea YESU wa kidini, akawaa mfuasi wa YESU tu,  lakini bado hajafunuliwa ndani yake!. Akamjua tu kulingana na dini ya kiyahudi kuwa atakuja Masihi na hivyo amemwona! Na si Zaidi.

  1. YESU WA UFUNUO.

Baada ya kipindi kirefu kupita, Petro ampokea YESU wa ufunuo na hapo inakuwa heri kwake.

Mathayo 16:13 “Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?

14  Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.

15  Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?

16 Simoni Petro akajibu akasema, WEWE NDIWE KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

17  Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni”.

Umeona hapo?… Petro amemjua YESU KIUFUNUO!.. aliyefunuliwa na Baba wa mbinguni, na si yule aliyeambiwa na kaka yake Andrea.

Kumbuka tayari alikuwa ameshajua kuwa YESU ndiye Kristo, kwani Andrea alishamwambia… Lakini ni kidini tu!..alipotulia na kumruhusu Roho Mtakatifu afanye kazi ndani yake ndipo akajua huyu wa kidini hatoshi, na kumbe YESU NA ZAIDI NA ALIVYOKUWA ANAMFIKIRIA..

Na utaona baada ya hapo ndipo Bwana anampa Petro funguo za Ufalme wa Mungu, baada tu ya kumpata YESU WA UFUNUO.

Mathayo 16:17 “Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni

18  Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

19  NAMI NITAKUPA WEWE FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI; NA LO LOTE UTAKALOLIFUNGA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGWA MBINGUNI; NA LO LOTE UTAKALOLIFUNGUA DUNIANI, LITAKUWA LIMEFUNGULIWA MBINGUNI”

Ni Kwanini leo hii, wengi funguo za ufalme wa Mungu hawana???… Sababu kuu ni YESU WALIYE NAYE MAISHANI MWAO si wa ufunuo bali wa kidini… Kama ni wa kidini huyo hawezi kufungua lolote ndani yao, lakini kama ni yule wa UFUNUO huyo anafungua mbingu na nchi!.

Sasa swali tunampataje YESU WA UFUNUO.

Tunampata YESU wa ufunuo kwanza kwa kuweka mbali mapokeo, na udini, na udhehebu na ujuaji na kumruhusu ROHO MTAKATIFU afanye ndani yako kwa unyenyekevu wote..huku ukiwa umejikana nafsi yako na kujitwika msalaba wako… Kidogo kidogo utaanza kumwona YESU kwa UFAHAMU MWINGINE, Na utayagundua mengi kumhusu yeye, na hayo mambo mapya utakayoyapata kumhusu YESU ndiyo mafunuo.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?

Petro na Adrea waliitwa na Bwana wakati gani?

HERI, WALE MUNGU ASIOWAHESABIA MAKOSA YAO.

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments