Je Bwana YESU alimjibu Pilato au hakumjibu? Je biblia inajichanganya?

Je Bwana YESU alimjibu Pilato au hakumjibu? Je biblia inajichanganya?

Swali: Je biblia inajichanganya kwa habari ya Bwana YESU kumjibu Pilato? Maana katika (Yohana 18:33-34) inasema alimjibu lakini katika (Mathayo 27:13-14)..  inasema hakujibu chochote alipoulizwa? Je lipi ni sahihi?


Jibu: Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa biblia haijichanganyi mahali popote pale, isipokuwa kinachojichanganya ni tafakari zetu, na fahamu zetu… Lakini biblia ni kitabu kikamilifu na kilichovuviwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, hivyo hakina kasoro yoyote.

Sasa tukirejea habari hiyo katika Yohana 18:33-37.

Yohana 18:33 “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?

34  Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?

35  Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini?

36  Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.

37  Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu”

Hapa ni kweli tunasoma Bwana YESU alimjibu Pilato alipoulizwa kuhusu habari zake mwenyewe… Lakini tukirejea kitabu cha Mathayo ni kama tunasoma habari tofauti kidogo.

Mathayo 27:11 “Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, WEWE WASEMA.

12  Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno.

13  Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni mambo mangapi wanayokushuhudia?

14  Asimjibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana”.

Hapa tunasoma Bwana YESU hamjibu Pilato.. Sasa swali je! Biblia inajichanganya??..Jibu ni la! Haijichanganyi.

Tukisoma vizuri habari hizo mbili zinaelezea kisa kimoja lakini katika mazingira manne tofauti..

  1. Mazingira ya Kwanza:

Wakati Bwana anafikishwa kwa Pilato, alitangulia liwali kumhoji Bwana YESU kama yeye ndiye mfalme wa Wayahudi hapo alijibu “wewe wasema (maana yake ndio mimi ndiye)” Huyo ni Liwali anahoji na anajibiwa na Bwana bila maficho yoyote.

Mathayo 27:11 “Naye Yesu akasimama mbele ya liwali; liwali akamwuliza, akasema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Yesu akamwambia, WEWE WASEMA…”

  1. Mazingira ya pili:

Lakini wakati ambao Wazee wa makuhani wanamshitaki Bwana YESU kwa Pilato yeye hakujibu chochote..

Kumbuka hapa wazee wa makuhani hawakuwa wanamhoji kuhusiana na swali alilouliza Liwali kwamba kama yeye ni mfalme wa Wayahudi…LA! Bali wazee wa makuhani wenyewe walikuwa wanamshitaki kwa mambo mengine ikiwamo habari ya kulivunja hekalu pamoja na kujiita mwana wa Mungu.. Soma Mathayo 26:62-68..Na sasa wanataka wamsikie Bwana YESU akijitetea mbele ya Pilato. Lakini Bwana YESU hakujibu chochote.

Mathayo 27:12  “Lakini aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu hata neno”.

  1. Mazingira ya tatu:

Pilato aliposimama na kumwuliza Bwana YESU ajitetee, mbele ya wazee wa makuhani kuhusiana na mashtaka hayo (ya kulivunja hekalu na kujiita mwana wa Mungu).. yeye hakujibu chochote mpaka Liwali akashangaa!!..

Mathayo 27:13 “Ndipo Pilato akamwambia, Husikii ni mambo mangapi wanayokushuhudia?

14  Asimjibu hata neno moja, hata liwali akastaajabu sana”

Na kwanini Bwana YESU hakumjibu hapa Pilato lolote?.. JIbu ni kwasababu Wazee wa Makuhani ambao waliokuwa ni wanafiki walikuwepo pale wakitafuta neno litokalo kinywani mwake ili waanze kuzusha maneno mengi juu yake..hivyo Bwana hakumjibu Pilato wala makuhani.

  1. Mazingira ya nne

Pilato alipoona hapati jibu lolote kuhusiana na mashtaka ya wayahudi juu ya Bwana.. alimchukua Bwana YESU ndani ya Praitorio na kumwoji akiwa peke yake swali lile lile aliloulizwa na Liwali! (Je wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?)..na Bwana YESU akampa jibu kama lile lile alilompa Liwali.

Yohana 18:33  “Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi?

34  Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu?…”

Umeona?… Kwahiyo biblia haijichanganyi yenyewe.. Ni kwamba Bwana YESU hakujibu mashtaka ya Wazee wa Wayahudi lakini alijibu maswali ya Pilato na Liwali.

Na kwanini Bwana YESU asijibu mashtaka ya wazee wa makuhani? Na amjibu Liwali pamoja na Pilato peke yao?…ni kwasababu wale wazee walikuwa wamemkusanyikia kwa shari, wapate kumwongezea dhiki….

Maswali yao si ya lengo la kutaka kujua, bali kutafuta sababu za kumshitaki..kwani tayari alishawajibu huko nyuma lakini bado waliendelea kumtafuta kwa maswali mengine mengi (Mathayo 26:62-68).

Kwahiyo na sisi tunachoweza kujifunza ni utulivu na kunyamaza katika vipindi ambavyo adui anatumia vinywa vya watu kutujaribu.. Ukishajibu swali mara ya kwanza, na mtu haelewi badala yake anatafuta tu kasoro, basi kinachofuata baada ya hapo ni kukaa kimya.

Kwasababu yapo maswali ambayo ukijibu hayatamsaidia yule anayeuliza badala yake yatampa kila sababu za kukusumbua wewe ziaidi, kwasababu lengo lake si kutaka kujua bali ni kubishana au kukudhuru wewe au kukushambulia. Hivyo ni muhimu kuwa makini.

Tito 3:9  “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana.

10  Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae”

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini maandiko yanajichanganya yenyewe kwenye habari ya Paulo alipotokewa na Yesu alipokuwa anakwenda Dameski?

Habari ile ya Pilato kuchanganya zile damu za wayahudi na pamoja na dhabihu zao,(Luka 13) ilihusu nini?

NENO LA MUNGU NI UFUNUO MKAMILIFU.

Liwali ni nani?

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest

2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Marshali Ezra sanga
Marshali Ezra sanga
10 months ago

Amen
Nafurahi kuhusu mnavyofundisha kweli ya MUNGU,Kwa kweli Mungu awabariki sana