Nini maana ya  “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)

Nini maana ya  “manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana” (Mathayo 11:13)

Jibu:Turejee,

Mathayo 11:12 “Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

13  KWA MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA”.

Mstari huo haumaanishi kuwa Torati yote na Manabii wote walimtabiri Yohana Mbatizaji.. kwamba atakuja kutokea na kuhubiri, na kwamba atakuwa nabii mkuu kuliko wote. Hapana, bali ilimaanisha kuwa Torati iliendelea kuwepo na kufanya kazi, na manabii waliendelea kutokea na kutoa unabii, mpaka wakati wa Yohana kutokea duniani.. na baada ya Yohana ndipo likaanza agano lingine jipya la ufalme wa Mungu kutangazwa na kila mtu kujiingiza kwa nguvu.

Maneno hayo yamewekwa katika Kiswahili kirahisi Zaidi katika kitabu cha Luka..

Luka 16:16  “Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu”.

Sasa kufahamu nini maana ya Torati na Manabii fungua hapa >>>Nini maana ya “Torati na manabii”?

Lakini ni kwanini aseme tangu wakati wa Yohana ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu na watu wanajiingiza kwa nguvu??..Ni kuonyesha kuwa hapo kwanza ilikuwa haiwezekani mtu kujiingiza katika ufalme wa Mungu..ilihitaji kuingizwa.. na waliokuwa wamesimama kama waingizaji wa watu katika ufalme wa Mungu ni Manabii na Torati..

Watu walisubiri maagizo ya Mungu kupitia Nabii au kuhani ndipo wapatanishwe na Mungu… lakini baada ya Bwana YESU kufa na kufufuka kiti cha rehema kimefunguliwa.. Watu hawahitaji tena manabii wala makuhani kumkaribia Mungu… (Maana yake kila mtu ana uwezo wa kumkaribia Mungu kupitia damu ya YESU).

Hatuhitaji tena kwenda Yerusalemu kwa makuhani ndipo tumsikie Mungu, hatuhitaji tena sanduku la agano, hatuhitaji tena nabii atokee ndipo atupe maagizo ya Mungu.. bali kupitia Roho Mtakatifu ndani yetu tunamkaribia yeye.

Kwa kadiri tunavyotia bidii ndivyo tunavyoukaribia na kuuteka ule ufalme..na wenye hekima na bidii ndio wanaoukaribia Zaidi ule ufalme.

Bwana atusaidie.

Maran atha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Mistari ya biblia kuhusu shukrani.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments