Je tunamwabuduje Mungu?

by Nuru ya Upendo | 18 September 2025 08:46 am09

Awali tufahamu nini maana ya kumwabudu Mungu, Kumwambudu Mungu si kumwimbia tu Mungu nyimbo ya kuabudu tulizozizoea, Neno kuabudu limetokana na neno “ibada” hivyo kumwabudu Mungu ni “kumfanyia ibada”

Sasa ibada imebeba mambo mengi ikiwemo kuomba, kumwimbia Mungu, kumtolea Mungu, kujifunza Biblia, kushiriki meza ya Bwana n.k

Sasa ni kwa namna gani tutamwabudu Mungu?.. si kwa njia nyingine zaidi ya hizo, ambazo ni kuomba ambako kunaweza kuhusisha kwa kupiga magoti au kusujudu, pia kumwimbia nyimbo za kumshukuru na kumsifu, na kumtolea matoleo yetu, na kujifunza maneno yake na kuyaishi na mambo mengine yanayoendana na hayo..

Maana yake tukiyafanya mambo hayo katika ukweli wote na katika roho bila kupunja chochote tutakuwa tunamwabudu Mungu..

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba kumwabudu Mungu ni kumfanyia Mungu ibada katika ukweli wote na katika roho, kwanini ni katika kweli yote na katika roho??..Turejee maandiko yafuatayo..

Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”.

Hivyo mpendwa kama unataka kumwabudu Mungu kweli kweli usikwepe kukusanyika kanisani, na hakikisha unakusanyika katika usafi na utakatifu, pia usikwepe ushirikia wa meza ya Bwana, pia usikwepe maombi binafsi na ya pamoja, usikwepe kumtolea Mungu (ni jambo la msingi sana), pia usikwepe kumshukuru Mungu na kumsifu kwa njia ya nyimbo na tenzi za rohoni.

Wakolosai 3:16 “Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

EPUKA KUCHELEWA IBADA.

NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.

NAWAAMBIA MAPEMA!

MWONGOZO WA MAOMBI YA ASUBUHI.

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/09/18/je-tunamwabuduje-mungu/