by Nuru ya Upendo | 20 December 2025 08:46 am12
Swali: Katika kitabu karibia chote cha Wimbo uliobora tunaona wakitajwa sana Binti za Yerusalemu je, hawa walikuwa ni mabinti wa aina gani?..au ni wa mji wa Yerusalemu kama Biblia inavyosema hapo?
Jibu: Turejee..
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, ENYI BINTI ZA YERUSALEMU, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.”
Sehemu nyingine Biblia inawaasa hawa Binti za Yerusalemu kutoyachochea mapenzi ..
Wimbo 2:7 “Nawasihi, enyi BINTI ZA YERUSALEMU, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”.
Sasa swali hawa Binti za Yerusalemu ni akina nani?
“Binti za Yerusalemu” au kwa lugha nyingine “Binti Sayuni” ni lugha ya mithali inayowakilisha “Jamii nzima ya watu wa Israeli”… na si Mabinti waliopo Yerusalemu tu peke yao..la! bali jamii yote ya wana wa Israeli.
Turejee maandiko yafuatayo ili tuweze kulielewa hili vizuri…
Zekaria 9:9 “Furahi sana, EE BINTI SAYUNI; piga kelele, EE BINTI YERUSALEMU; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.”
Unabii huu ulimuhusu Bwana YESU kipindi anaingia Yerusalemu, ambapo jamii ya watu wote walipomwona walikata majani ya mitende na kutandaza njiani ili apite..
Yohana 12:15 “Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;
13 wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, HOSANA! NDIYE MBARIKIWA AJAYE KWA JINA LA BWANA, MFALME WA ISRAELI!
14 Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa,
15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.
16 Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo”.
Umeona hapo?.. waliooimba Hosana! Hosana! si tu mabinti waliokuwepo Yerusalemu bali “ni jamii yote na marika yote!”.. ikifunua kuwa Binti za Yerusalemu ni jamii nzima wa Israeli, kuzidi kulithibitisha hilo soma pia Mika 4:8, 2Wafalme 19:20-21, Isaya 37:22, na Isaya 62:1.
Na sisi kama wakristo (wakike na kiume) tunahesabika kama Israeli ya Rohoni, hivyo sisi sote pasipo kujalisha jinsia zetu, marika yetu wala nafasi zetu, maadamu tu tumempokea YESU tunafahamika kama Binti Sayuni, au Binti za Yerusalemu.
Na Biblia inatuonya Binti za Yerusalemu, mji wa Mungu tujiepushe na dhambi, hususani Uasherati wa rohoni na mwilini.
Uasherati wa rohoni ni ibada zote za sanamu.. Je umempokea BWANA YESU KRISTO?.
Fahamu kuwa hizi ni siku za Mwisho na YESU amekaribia sana kurudi.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Machela ni nini (Wimbo ulio bora 3:7)
Pambaja ni nini katika Biblia kama tunavyosoma katika kitabu cha Wimbo ulio bora 1:2?
MAAJABU YA AGANO LA UPENDO WA KRISTO.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2025/12/20/binti-za-yerusalemu-wanaotajwa-katika-kitabu-cha-wimbo-ulio-bora-15-ni-akina-nani/
Copyright ©2026 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.