Jibu: Pambaja ni neno linalo maanisha “upendo” (ule wa mwanaume na mwanamke). Upo upendo wa ndugu kwa ndugu, mfano upendo wa Mzazi na mtoto, dada na kaka wa familia moja na pia upo upendo wa mwanamke na mwanamke. Sasa upendo huu wa mwanaume na mwanamke kwa lugha nyingine ndio unaoitwa PAMBAJA. Neno hili linaweza kutumika kama wingi, lakini linamaanisha vile vile upendo.
Wimbo ulio Bora 1: 2 “Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai”
Wimbo ulio Bora 4: 10 “Jinsi zilivyo nzuri pambaja zako, umbu langu, Bibi arusi, ni nzuri kupita divai; Na harufu ya marhamu yako Yapita manukato ya kila namna”
Pia unaweza kulipata neno hilo kwenye mistari hii; Wimbo 1:4, Wimbo 7:12.
Sasa ni kwanini upendo huu umetajwa hapo?, je una umuhimu wowote kwetu sisi wakristo?. Ndio una umuhimu mkubwa, kwanza kwa wana-ndoa na Pili kwa Kristo na Kanisa lake.
Kumbuka Sisi wakristo katika roho tunafananisha na bibi-arusi na Kristo ndiye Bwana Arusi. Hivyo jinsi Kristo anavyolipenda kanisa upendo wake ni kama wa mke na mume (yaani Pambaja). Na kama unavyojua wivu ni mbaya kuliko ghadhabu..Na ndivyo Kristo anavyotuonea wivu, tunapoiacha njia ya haki na kuufuata ulimwengu.. Tunamtia wivu.
Wimbo 8: 6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu”
Hivyo sisi tuliookoka ni watu wa thamani mbele ya Kristo, ni bibi-arusi wake, anayetupenda na kutujali na katuandalia mambo mengi mazuri mbinguni katika karamu yake aliyotuandalia..
Ufunuo 21: 9 “Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu”
Ufunuo 21: 9 “Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu”
Je utaikosa hiyo Yerusalemu mpya iliyoandaliwa mahususi kwa bibi-arusi?. Kama hujampokea Kristo hutaurithi uzima huo wa milele. Hivyo mpokee leo, kwa kutubu na kwenda kubatizwa na yeye atakupokea.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
JE! UKIMWI UNATIBIKA?
JIKANE NAFSI MTEULE WA MUNGU.
BWANA SI MWEPESI WA HASIRA, LAKINI BWANA NI MWINGI WA HASIRA.
Rudi nyumbani
Print this post