Jibu: Turejee…
Wimbo 3:7 “Tazama, ni MACHELA yake Sulemani; Mashujaa sitini waizunguka, Wa mashujaa wa Israeli”
“Machela” yanayozungumziwa hapo si vile vitanda vinavyotumika zama hizi kwaajili ya kubebea wagonjwa walio mahutihuti!..Bali vilikuwa ni vitanda maalumu vilivyotumika kubebea Wafalme na Mamalkia enzi za zamani, walipotembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine (umbali mfupi).
Kutokana na zama kubadilika, matumizi ya Machela kubebea wakuu wa nchi hayapo tena, bali sasa yanatumika magari ya kimakenika, na Machela yamebaki kuwa na matumizi ya kubebea wagonjwa wa dharura walio katika hali ya umahutihuti,..na zaidi sana Machela za zama hizi yana magurudumu na hayabebwi tena kwa mikono kama yale ya zamani.
Kasoro moja ya Machela ya zama za zamani ambayo yaliwabeba wafalme ni kwamba hayakuwa na uimara wa kutosha, kiasi kwamba ikitokea ajali kwa waliombeba bali yule aliyebebwa anaweza kuanguka, na pia kwasababu mwendo wa wanadamu unatofuatiana, hivyo basi hata aliyebebwa wakati wa safari atahisi hali ya kupanda na kushuka, au kurushwa rushwa, na kupepesuka na hivyo yupo hatarini saa yoyote kuanguka..
Na vivyo hivyo, dunia imefananishwa na mfalme aliyebebwa kwenye machela, anawaya-waya, anapepesuka wakati wowote yupo hatarini kuanguka (yupo katika wasiwasi).
Isaya 24:19 “Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana. 20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, NAYO INAWAYA-WAYA KAMA MACHELA; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena. 21 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia”
Isaya 24:19 “Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana.
20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, NAYO INAWAYA-WAYA KAMA MACHELA; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.
21 Tena itakuwa katika siku hiyo, Bwana ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia”
Kama dunia inawaya-waya, ya nini kuitumainia??.. Na kwanini inawaya-waya?..ni kwasababu imekaribia mwisho wake, wakati wowote inaisha…na kinachoifanya iwayewaye si kingine Zaidi ya Dhambi, iliyojaa ndani yake.
Kwa urefu zaidi kuhusu kuwaya-waya kwa dunia fungua hapa >>> Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
Je umempokea YESU maishani mwako?..au na wewe unawaya-waya na dunia?…anasa zimekutawala, udunia umekushika..ni wakati sasa wa kuikimbia dunia na mambo yake na kumfanya BWANA YESU kuwa msingi wa maisha yako.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
TOA HUDUMA ILIYO BORA.
Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
KWA KUWA ROHO BORA ILIKUWA NDANI YAKE.
Kimiami ni nini? (Wimbo ulio bora 2:9).
INGIENI KWA KUPITIA MLANGO ULIO MWEMBAMBA.
Rudi Nyumbani
Print this post