Maana ya  Yakobo 1:17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu,

Maana ya  Yakobo 1:17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu,

SWALI: Naomba kufahamu tafsiri ya Yakobo 1:13-17, hususani pale anaposema “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu”

Yakobo 1:13-17,

[13]Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. 

[14]Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. 

[15]Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. 

[16]Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. 

[17]Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. 


JIBU: Katika hiyo mistari ya juu kabisa, tunasoma mtume Yakobo akitoa ufafanuzi wa mawazo ya watu kuhusu Mungu ambayo sio sahihi. Wakidhani kuwa majaribu yampatayo mtu hutolewa na Mungu, kwasababu chanzo chake ni Mungu.

Chukulia mfano labda mpendwa kabarikiwa na Mungu kwa shamba la mizabibu, likawa linasitawi sana, hata kumfanya afungue kiwanda chake cha juisi na kuuza na kupata faida nyingi..Sasa baada muda fulani watu wakamfuata na kuulizia bidhaa ya mvinyo, mwanzoni alikataa, lakini baadaye alipopiga hesabu na kuona faida itakuja mara nne,.akaingiwa na tamaa akaanza kutengeneza divai akauza na yeye mwenyewe akaanza kuwa mlevi, hatimaye maisha yake ya wokovu yakaporomoka akawa amekufa kabisa kiroho. Mwishowe akaanza kumlaumu Mungu amemletea jaribu la kumpa shamba la mzabibu na kumbariki sana, ndio maana akawa mlevu.  Sasa mtu wa jinsi hii Mtume Yakobo anasema asiseme amejaribiwa na Mungu.

Ni sawa na tamaa za mwili,.Mungu aliziweka mahususi kwa ajili ya furaha ya wanandoa lakini imebadilika na kuwa uzinzi, na watu hutumia kisingizio kuwa Mungu ameziweka kama jaribu kwao. kumbe Mungu alichowapa ni chema isipokuwa wao wenyewe wamekigeuza kuwa uovu.

ndo maana sasa ya vifungu vinavyofuata vinasema. “kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu. Kwa lugha rahisi anamaanisha chochote kitolewacho kilicho chema hutoka kwa Mungu, lakini tu sio kilicho chema bali pia chochote kilicho kikamilifu, hutoka juu kwa Baba yetu.

Mungu sikuzote hutupa sisi vitu vizuri. Na si vizuri tu bali pia vilivyo vikamilifu hutoka kwake. tujengwe na tufurahie, isipokuwa sisi huvipindua na kuvitumia kwa tamaa zetu. 

Pesa ni kitu kizuri, chakula ni kitu kizuri, usingizi ni kitu kizuri, ndoa ni kitu kizuri, kazi ni kitu kizuri, muziki ni kitu chema.

Lakini watu wanapovitumia kinyume ndio huzaa uzinzi, anasa, ulevi, uvivu, ufisadi.n.k.

Vitu vyote vyema vimetoka kwa Mungu na hajatupa ili kutujaribu..anaendelea kusema..

“hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka”. 

Baba wa mianga, akijifananisha na jua ambalo huangaza kotekote, isipokuwa yeye amelizidi jua, hana misimu wala majira ya kuangaza, yeye wakati wote hutoa vilivyo vyema, hifadhili majira yote kwa watu wake.

Hata leo, uonapo Mungu amekupa kitu chema, halafu baadaye kikakuletea matatizo makubwa.. Tafakari hapo kuna mahali ulimpa nafasi shetani kukujaribu. Kwasababu Mungu hawezi kumpa mtu jiwe aliyemwomba mkate.

“kila kutoa kuliko kwema na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

YAFAHAMU MAPENZI KAMILI YA MUNGU KWA MAADUI ZAKO.

EPUKA KUTOA UDHURU.

SI KILA KILICHO HALALI KINAFAA.

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments