Yuaabisha kichwa chake! Je ni aibu ya namna gani? (1Wakorintho 11:5)

Yuaabisha kichwa chake! Je ni aibu ya namna gani? (1Wakorintho 11:5)

Jibu: Turejee..

1Wakorintho 11:3 “Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

4  Kila mwanamume, asalipo, au anapohutubu, naye amefunikwa kichwa, yuaaibisha kichwa chake.

5  Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, YUAAIBISHA KICHWA CHAKE; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa”.

Kuhusiana na maelezo marefu juu ya agizo la wanawake kufunika vichwa wawapo ibadani fungua hapa >>>Je! Mwanamke anapaswa afunikwe kichwa anapokuwa ibadani?

Lakini matokeo ya Mwanamke kutofunika kichwa awapo ibadani ni “kuabisha kichwa chake”. Na kichwa kinachozungumziwa hapo (kinachoaibika) si kile chenye nywele bali ni kile cha “UONGOZI”

Kwahiyo mwanamke asipofunika kichwa chake awapo ibadani, kulingana na biblia anaaibisha Uongozi aliowekwa chini yake na Roho Mtakatifu!, Na uongozi huo si mwingine Zaidi ya ule  wa zile huduma tano zinazotajwa katika Waefeso 4:11 (Mitume, Manabii, Waalimu, Wachungaji,  na wainjilisti)…ambazo ni huduma za wanaume tu!. (Kumbuka tena, si agizo la biblia mwanamke kuwa mchungaji!, rejea Zaidi 1Wakorintho 14:34, na 1Timotheo 2:11-12.

Na matokeo ya kuuabisha huo uongozi wa Roho Mtakatifu ni kumwaibisha KRISTO mwenyewe kwasababu pia Kichwa cha kila mwanaume (yaani uongozi wa kila mwanaume anayemtumikia Mungu) ni KRISTO (sawasawa na hiyo 1Wakorintho 11:3). Hivyo mwanamke ni lazima afunike kichwa chake awapo ibadani, kama dalili ya kuongozwa (kumilikiwa).

Sasa swali lingine ni hili, Je Mwanaume naye anapaswa afunike ili asimwaibishe Kristo?…Jibu ni la!.. Mwanaume hapaswi kufunika kichwa awapo kanisani, Kwasababu yeye ni mfano wa Utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa Mwanaume..

1Wakorintho 11:7 “Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume”.

Anaposema mfano wa Utukufu wa Mungu, maana yake “yeye anasimama kumwakilisha KRISTO” amepewa hiyo nafasi ya kuwa mwakilishi wa KRISTO kwa neema, (Ingekuwa hajapewa hiyo nafasi, basi na yeye pia ingempasa afunike kichwa) lakini kwasababu kapewa nafasi ya kumwakilisha KRISTO, basi hapaswi kufunika kichwa, bali anapaswa awe kama KRISTO,

Maana yake kama Kristo alivyo Mchungaji, naye pia atakuwa mchungaji, kama Kristo alivyo mwalimu, naye pia atakuwa mwalimu, n.k. Lakini mwanamke hajapewa hiyo nafasi ya kumwakilisha KRISTO kwasababu hajaumbwa kwa mfano wa utukufu wa Mungu, bali kwa utukufu wa Mtu (mwanaume).

Kwahiyo kama wewe ni Mama, au dada, basi fuata agizo hilo la Bwana YESU wala usikubali kiburi cha kidunia kikuvae, kwa kufikiri hayo ni maagizo ya wanadamu au ni sheria ya torati..hiyo sio sheria bali ni agizo la Bwana tena lipo katika agano jipya.. na Zaidi sana Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho Mtakatifu alijua fitina zitazuka kushindana na agizo hilo siku za mwisho..

1Wakorintho 11:16 “Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu”.

Bwana atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)

FUVU LA KICHWA.

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

Biblia inasemaje kuhusu Nywele?

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments