Na kipenu ni nini (Isaya 1:8)

by Nuru ya Upendo | 5 January 2026 08:46 am01

Jibu: Turejee..

Isaya 1:8 “Na binti Sayuni ameachwa kama kibanda katika shamba la mizabibu, kama KIPENU katika shamba la matango, kama mji uliohusuriwa”.

“Kipenu” ni kijumba kidogo kinachojengwa katikati ya Shamba, kinachomsitiri mlinzi wakati wa kulinda mazao shambani..

Ili kuzuia wezi wa mazao, na wanyama kama nyani, ngedere na wengineo pamoja na ndege inawalazimu wakulima kuweka walinzi mashambani, ili kuyaangalia mazao hayo, sasa kile kijumba cha walinzi, ambacho kinajengwa kwa ubora wa chini kwa kusudi hilo, ndicho kinachoitwa “Kipenu”.

Mara nyingi kijumba hiki, pale ambapo uvunaji umemalizika, huwa kinabaki chenyewe shambani wala hakuna mtu anakithamini tena, wanyama wanaweza kufanya makao huko na hakina thamani tena…… hali hii ya kipenu kusalia chenyewe shambani, na kupoteza uthamani wake ndio Bwana MUNGU anafananisha na jinsi Mji wa Yerusalemu (yaani binti Sayuni) ulivyoachwa..

Kutokana na maovu kuwa mengi Yerusalemu, na Bwana aliwaacha, na mji wao kubaki mpweke kama kipenu, na hivyo hatari yoyote inaweza kuukabili, na ndicho kilichotekea wakati ulipofika Yerusalemu uliachwa kama Kipenu na Nebukadreza, mfalme wa Babeli  aliuhusuru na kuuharibu na kuwachukua wenyeji mateka.

Hata sasa tunapomwacha MUNGU, tunakuwa kama Kipenu katikati ya shamba lililokwisha kuvunwa. Nyumba zetu zitakuwa kipenu, roho zetu zitakuwa kama kipenu, biashara zetu zitakuwa kama kipenu na mambo yetu mengine yote yatafananishwa na vipenu.

Hautaweza kuilinda roho yako, wala nyumba yako kama utakuwa nje ya Kristo, ni lazima tu uharibifu wako utafika ghafla siku moja, Mwanadamu ameumbwa kumtegemea MUNGU siku zote, kamwe hawezi kuishi kwa kujitegemea mwenyewe, ni jambo ambalo haliwezekani na gumu sana. Bwana tu ndiye tegemeo letu na ngao yetu.

Zaburi 144:2“Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu”.

Bwana atubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE

MAVUNO YAMESHAKWISHA  SHAMBANI.

USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

WhatsApp
DOWNLOAD PDF

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2026/01/05/na-kipenu-ni-nini-isaya-18/