MAVUNO YAMESHAKWISHA  SHAMBANI.

MAVUNO YAMESHAKWISHA  SHAMBANI.

Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.

Bwana Yesu asifiwe ndugu mpendwa..

Ukitaka kujua kuwa mambo yote sasa yameshakamilika, kinachongojewa ni UNYAKUO tu, angalia hali ya mavuno shambani mwa Bwana. Embu fananisha watu waliokuwa wanamjia Kristo kipindi cha mitume, na watu wanaookoka sasa  katika kipindi chetu hichi.

Kipindi kile injili ilipokwenda kuhuburiwa mahali kwa mara ya kwanza, mwitikio wa watu  wa kumgeukia Kristo ulikuwa ni wa kustaajabisha sana, utakumbuka baada ya Pentekoste tu, kanisa lilikuwa likijiongeza  kwa idadi ya maelfu, kwa injili ndogo sana. Na ndio maana kwa kipindi kifupi sana, ukristo ulienea ulimwenguni kote, na sio kuenea tu, badi kuhubiriwa (Wakolosai 1:6, 1Wathesalonike 1:8).Hiyo ni kuonyesha kuwa kweli ule ulikuwa ni wakati wa mavuno.

Lakini angalia sasa,  mambo ni tofauti hakuna mtu asiyeifahamu injili, au kuzijua habari za Kristo, wote tunazifahamu, lakini jiulize kwanini, watu hawataki kuokoka, kinyume chake ndio wanakwenda mbali kabisa na Ukristo..Hiyo ni kuonyesha kuwa mavuno yameshakwisha shambani, kilichobaki ni magugu tu.

Na hiyo imepelekea sasa injili kubadilika sio tena ya kuwavuta watu, bali ni ya ushuhuda. Unapoona, injili imekufikia hapo ulipo kitandani kwako ukiwa umeishika simu yako na kusoma, ujue hiyo sio ya kukuvuta wewe, hiyo ni ya ushuhuda tu, ukiona injili imekufikia hapo sebuleni kwako unapotazama tv na familia yako, injili inakufikia kwenye hivyo vipeperushi unavyovisoma huko mitaani. Unapewa biblia bure ya kwenye simu yako, mambo ambayo hata zamani hayakuwepo. Basi ujue hiyo sio injili ya kukuvuta tena kwa Kristo ndugu. Ni injili ya USHUHUDA Tu. Ili utakapokufa katika dhambi zako, usiwe na sababu ya kusema sikuwahi kusikia, au kuona, au kuambiwa.

Wewe jiulize tu, ni kwanini pamoja na mahubiri yote hayo uliyohubiriwa na kuyasikia siku zote za maisha yako, na bado huna badiliko lolote ndani yako. Unadhani ni jambo la kawaida? Hapana, kwa kawaida Neno moja tu lingetosha kukufanya uwe mtakatifu sawasawa na Waebrania 4:12.  Lakini hujageuka kwasababu  wewe sio Ngano bali ni gugu tu.

Kilichosalia sasa hivi ni Mungu anatazama walau kama yatakuwepo masalia salia machache ayaokoe. Lakini nataka nikuambie, moja ya hizi siku ambazo zinahesabika, tutashuhudia mabadiliko makubwa sana duniani. Tutashuhudia tendo kuu la Unyakuo wa kanisa.

Ndio yale maneno ambayo Bwana Yesu alisema, .(Mathayo 24:40-42) yatatimia hapo. Usiku huo wawili watakuwa wamelala mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wanasaga(ikimaanisha watakuwa katika biashara zao), mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa. Wale watakaoachwa, huku duniani kitakachokuwa kinaendelea ni vilio na kusaga meno. Wakijuta kwanini kipindi kile hawakuitii sauti ya Mungu, ilipokuwa inawavuta kwake kwa upole. Watalia na kuomboleza, kweli kweli, ndugu usiwe mmojawapo.

Lakini watakaokuwa wamenyakuliwa, moja kwa moja wataelekea mbinguni wakiwa na miili yao ya utukufu, katika ile karamu ya mwana-kondoo.  Kwenye raha isiyokuwa na kifani. Wakifutwa machozi kwa taabu zao walizokuwa wanapitia huku duniani kwa ajili ya Kristo.

Ndugu mambo haya unaweza kuona kama ni hadithi, au mambo yatakayotokea miaka elfu 5 mbeleni, usijidanganye. Yesu aliposema TUBUNI, kwa maana ufalme wa mbinguni UMEKARIBIA. Alikuwa hasemi uongo. Ni kweli ufalme wa mbinguni  ulikuwa umekaribia, jiulize  sisi wa sasa hivi tusemeje?.

Maanisha kugeuka, unaposikia injili kwa wakati huu.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

UNYAKUO.

KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!

MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.

UFUNUO: Mlango wa 14

Kuwiwa maana yake nini katika biblia?

Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments