Neno hilo utalisoma kwenye vifungu hivi katika biblia;
Walawi 12: 3 Siku nane mtoto atatahiriwa govi ya zunga lake.
Kutoka 4:24 “Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, Bwana akakutana naye akataka kumwua. 25 Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi”.
Kutoka 4:24 “Ilikuwa walipokuwa njiani mahali pa kulala, Bwana akakutana naye akataka kumwua.
25 Ndipo Sipora akashika jiwe gumu na kuikata govi ya zunga la mwanawe, na kuibwaga miguuni pake akasema. Hakika wewe u bwana arusi wa damu kwangu mimi”.
Zunga ni kipande cha govu kilicho mbele ya maumbile ya mwanaume. Pale anapotahiriwa kipande hichi cha nyama ndicho kinachoondolewa. Hicho ndicho kinachojulikana kama Zunga.
Mungu alitoa maagizo kwa Ibrahimu na wazao wake wote, kuwa watahiriwe, kwa kukatwa zunga zao. Na kwamba hiyo ndio itakuwa dalili ya agano aliloingia nao, siku zote za maisha yao.
Mwanzo 17:9 “Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. 10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. 12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako”.
Mwanzo 17:9 “Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.
10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa.
11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako”.
Mwanzoni Ibrahimu wala wa Israeli hawakuelewa ufunuo wa Mungu kuwaambia wafanye vile. Lakini sisi tuliomwamini Kristo leo hii ndio tunaofahamu kuwa. Kumbe kila mwanadamu anazaliwa na zunga lake la asili(yaani dhambi ya asili) rohoni. Na kwamba linapaswa litoke, kwa kukatwa. Na linaondolewa kwa kumwamini tu Yesu Kristo, ambapo kunaambatana na kubatizwa katika ubatizo sahihi.
Wakolosai 2:11 “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. 12 Mkazikwa pamoja naye KATIKA UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.
Wakolosai 2:11 “Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo.
12 Mkazikwa pamoja naye KATIKA UBATIZO; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu”.
Unaona, usipotahiriwa moyo wako, wewe huna agano na Mungu. Hivyo kwasasa tohara yetu sio tena ya mwilini, bali rohoni, Na kila mmojawetu ni sharti awe nayo.
Wafilipi 3:3 “Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili”.
Swali ni Je! Umeokoka? Je! Umebatizwa ipasavyo?. Kumbuka ubatizo sahihi ni muhimu katika ukristo wako, na tohara yako ya rohoni kama tulivyosoma hapo juu. Yakamilishe maagizo yote ya Bwana Yesu, kwasababu hatuokoki kwa kukiri tu bali pia na kwa kubatizwa, na ubatizo ni sharti uwe wa kuzamishwa kwenye maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na Matendo 2:38, 8:16:, 10:48, 19:5
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
JE! ULEVI NI DHAMBI?.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 10 (Kitabu cha Zaburi).
WAPE WATU WANGU RUHUSA ILI WAPATE KUNITUMIKIA.
Vyombo vya uzuri ni vipi vinavyotajwa katika biblia?
Rudi nyumbani
Print this post