Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? Ina maana gani?

by Admin | 30 August 2019 08:46 pm08

Biblia inaposema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika? ” Swali ni Je! sisi tutawahukumu vipi Malaika?.

1Wakorintho 6:2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?

JIBU: Watakatifu wamefananishwa na BWANA wetu YESU KRISTO kwa sababu yeye aliitwaa asili ya mwanadamu na sio asili ya malaika wala kiumbe kingine chochote, maandiko yanamtaja yeye kama mzaliwa wa kwanza kati ya ndugu wengi (ambao ndio sisi),

Waebrania 2:16 ” Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.

17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake”.  

Unaona hapo na kama vile Mungu alivyompa vitu vyote vya mbinguni, na vya duniani na vya kuzimu vivyo hivyo alimpa pamoja na hukumu yote (Yohana 5:22), na pia tukisoma:  

Waefeso 1:20 “aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;

21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;

22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo

23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” 

Kwahiyo kama Mungu amempa vyote ikiwemo na hukumu ya viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani, visafi na vichafu, vilivyopo na vitakavyokuja, hivyo ni dhahiri kuwa malaika wote watakatifu na walioasi wapo chini yake na watahukumiwa na yeye kulingana na njia zao, aidha ni nzuri au mbaya, kwa mfano ule ule atakavyowahukumu wanadamu wote watakatifu na waovu.Hivyo basi kama watakatifu watakuja kuketi pamoja na KRISTO (Ufunuo 3:21) ni wazi kuwa watahukumu pamoja na Kristo, maana wakati huo watasimama kama ndugu zake.   Na ndio maana Mtume Paulo anaoujasiri wa kusema hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika

Kwahiyo ndio ni kweli malaika wote watahukumiwa na watakatifu, wale malaika watakatifu watazidi kutukuzwa zaidi pamoja na Kristo katika umilele ujao, na wale waovu (shetani na malaika zake) watahukumiwa na kutupwa katika lile ziwa la moto pamoja na wanadamu walioasi. kumbuka hizi hukumu zitafanywa na YESU pamoja na watakatifu wake tu!. Na ndio maana maandiko yanasema tutauhukumu ulimwengu na malaika wote.

Ufunuo 20:4 inasema…

” KISHA NIKAONA VITI VYA ENZI, WAKAKETI JUU YAKE, NAO WAKAPEWA HUKUMU; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.”

 Kwahiyo wale tu watakaoshinda na KUKETI PAMOJA NAYE KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI hao ndio watakaohukumu ULIMWENGU na MALAIKA. Amina.   Kumbuka watakaokuwa na mamlaka hayo ni wale watakaoshinda tu (watakaonyakuliwa)..  Na mamlaka hayo tutayapata baada ya kumaliza maisha haya, lakini kwa sasa tumewekwa chini ya malaika, kama Bwana Yesu alivyowekwa chini yao kipindi yupo duniani (Waebrania 2:9 ) mpaka alipomaliza kazi na kutukuzwa..Kwahiyo tujitahidi tushinde maana biblia inasema..

Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

 JE! MBINGUNI KUNA MALAIKA WA KIKE?. NA JE! TUKIFIKA MBINGUNI TUTAFANANA WOTE?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

 JE! KUNA MALAIKA WA AINA NGAPI?

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/biblia-inasema-hamjui-ya-kuwa-mtawahukumu-malaika-je-sisi-tutawahukumuje-malaika/