Malaika wa maji ni yupi na Je kuna aina ngapi za malaika?

Malaika wa maji ni yupi na Je kuna aina ngapi za malaika?

SWALI:Katika kitabu cha Ufunuo 16:5, Tunaona akitajwa malaika wa maji ” Swali Huyu malaika wa maji ni nani? Naje! Kuna malaika wa aina ngapi?

JIBU: Ulimwengu wa malaika ni mkubwa/Mpana sana kama vile ulivyo ulimwengu wa wanadamu, Kama vile Mungu alivyotoa vipawa tofauti tofauti kwa wanadamu, vivyo hivyo alitoa vipawa tofauti tofauti kwa malaika zake,..wapo malaika wa maji,(hawa wanashughulika na mambo yote yanayohusiana na maji,mfano kuleta gharika kama wakati wa Nuhu,kutenganisha bahari kama wakati wa Musa,kusababisha au kuzuia mvua kama wakati wa Eliya , kutokeza maji mwambani kama wakati wa Wana wa Israeli jangwani, kutokeza chemichemi, kugeuza maji kuwa kitu chochote kama damu n.k.)..Na watakuja kufanya hizo kazi tena katika siku ile kuu ya Bwana baada ya kanisa kunyakuliwa..Wapo pia malaika wa moto (utawaona katika..

Ufunuo 14: 18 “Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana”

 Wapo pia Malaika wa vita, mfano Mikaeli na wenzake,kazi yao ni kudhibiti nguvu za yule adui kwa watakatifu wa Mungu, wapo malaika wajumbe kama Gabrieli na wenzake (Danieli 9:21) ambao kazi zao ni kuwasilisha ujumbe fulani kutoka kwa Bwana kwa watakatifu, na wapo pia wa sifa (makerubi na maserafi) na shetani naye alikuwa kwenye hili kundi kabla ya kuasi, n.k.Hawa wapo mbele ya kiti cha Enzi cha Mungu milele,

Isaya 6: 1 “Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake”. 

kwahiyo wapo wengi hata wengine hatuwajui, na wala hatujawahi kuwaona, wapo wanaoshughulika na ULINZI tu,soma Zaburi 91: 11 “Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote”.

Kutoka 23:20 “Tazama, mimi namtuma malaika aende mbele yako, ili akulinde njiani na kukupeleka mpaka mahali pale nilipokutengezea.”

Wapo malaika wa kila nchi, wapo wa kila mkristo mmoja mmoja, na wapo wanaosimama kwa kila huduma, n.k kila mmoja anatenda kazi kulingana na alivyopangiwa na Mungu mwenyewe…Wapo pia malaika wa Uponyaji, (Yohana 5:15). 

Na karama nyingi za rohoni zinachochewa na hawa malaika wanaotembea na watakatifu. Kwamfano karama za upambanuzi wa roho,miujiza n.k.(Waefeso 4:8) Lakini hawa wote hawaonekani kwa macho, ni viumbe wa rohoni,(japo wakati mwingine wanaweza wakaonekana kwa macho) ndio maana MUNGU WETU ANAITWA BWANA WA MAJESHI! unaweza ukajiuliza hayo majeshi ni akina nani??? sio wanadamu kwasababu wanadamu sisi tunaitwa WANA WA MUNGU (Waebrania 1:5).. Bali ni malaika ndio wanaoitwa MAJESHI ya BWANA…yapo MAELFU kwa MAELFU ya malaika wanazunguka kila siku duniani kuwahudumia watu wa Mungu (Waebrania 1:13-14).Inasema..

“ 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?”.

 Kwahiyo uwezekano wa mtu kuzungukwa na wingu kubwa la malaika kama ilivyokuwa kwa Nabii Elisha inategemea na kiwango cha utakatifu wake na kiwango chake cha kulitii Neno la Mungu. Kwasababu hawa wanafanya kazi katika kanuni za Neno la Mungu tu! Nje ya hapo! Wanakuwa Hawana msaada wowote kwako..Kwamfano Neno la Mungu linaposema waheshimu Baba yako na mama yako upate siku nyingi za kuishi duniani..

Sasa mtu anapolishika hilo NENO kwa bidii , wale malaika wanaohusika na ulinzi, wanatumwa kuhakikisha kwamba maisha yako hayaathiriwi ni kitu chochote kile mpaka ule umri utakapotimia ndio hapo utakuta hata ikitokea ajali ya namna gani wanaweza wakafa watu wote yeye ukapona, au labda magonjwa Fulani yanaowapata wazee kama upofu,n.k., utashangaa wengine wanayapata lakini yeye hayakupati, ni kwasababu umelishika lile Neno hivyo siku zote anakuwa anazungukwa na jopo kubwa la malaika..

Kadhalika na ahadi zote za Mungu vivyo hivyo zinaambatana na Malaika wa Bwana. Lakini kama hutaishi kulingana na Neno la Mungu, ina maana kuwa hao malaika watakuwa hawapo, kinyume chake mapepo ndio yatachukua nafasi zao, ndio unaweza kushangaa, mtu anakufa kabla ya wakati wake, wachawi wanamloga, wengine magonjwa yasiyoeleweka, wengine mikosi n.k. Kwahiyo jambo kubwa linalofukuza uwepo wa malaika ni dhambi katika maisha ya mtu.

 Ubarikiwe sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?

JE SISI TUTAWAHUKUMUJE MALAIKA?

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

NINI MAANA YA ELOHIMU?

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
5 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Emmanuel Kitengule
Emmanuel Kitengule
1 year ago

Barikiwa sana mwalimu.Ninakuelewa vilivyo.

M
M
1 year ago

Amina

Maige
Maige
2 years ago

Amen…Tuzidi sana kuishi Maisha matakatifu. Habari njema.

Sauli
Sauli
3 years ago

Napendelea kufuatilia mafundisho haya.