Je! mtu aliyeokoka anaruhusiwa kumiliki Lodge ambayo ina Bar ndani yake?

by Admin | 30 August 2019 08:46 pm08

Swali linaendelea….na kutoa fungu la kumi kwa kupitia hiyo?,kwa mfano mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kampuni ya TBL kazi ya kampuni hii ni kutengeneza na kuuza bia kama yalivyo makampuni mengine kama Serengeti nk. Huyu ndugu ni mkristo aliyeokoka na jumapili bila shaka hutoa fungu la kumi na sadaka zingine pia ana cheo kanisani ..je! ni kuna makosa yoyote kufanya hivyo?


 

JIBU: Kumiliki bar ni dhambi, vilevile kumiliki lodge lenye bar ni dhambi..biblia inasema wazi katika

Kumbukumbu 23:18 “usilete ujira wa kahaba wala mshahara wa mbwa katika nyumba ya Bwana, ni machukizo”

Kumbuka na sio tu kazi ya bar tu, bali hata na kazi nyingine yoyote isiyokuwa halali mfano biashara ya madawa ya kulevya, ufisadi, ulanguzi,uuzaji pombe,wizi, kamari, uuzaji sigara n.k kamwe usijaribu kufanya hivyo ukadhani kuwa Mungu ataziridhia sadaka zako, hata kama unatoa nyingi kiasi gani au kwa moyo kiasi gani, kwa kufanya hivyo utakuwa unajichukulia laana badala ya baraka, ni machukizo mbele za BWANA, kutii ni bora kuliko dhabihu(1 Samweli 15:22) Mungu ni mtakatifu na sio mtaka-vitu.

Kwahiyo unapokwenda mbele zake ni vema kufahamu kuwa yeye ni Mtakatifu na anaihitaji roho yako sana zaidi ya vitu vyako. Kwahiyo kuhusu hiyo kazi anapaswa aache,kwasababu biblia imeturuhusu kiungo chetu kimoja kikitukosesha tuking’oe. kumiliki bar ni dhambi..Hivyo amwombe tu Mungu awe mwaminifu atampa kazi nyingine tena nzuri zaidi ya hiyo.. Mungu Alisema kuwa anajua tunayahitaji hayo yote

Mathayo 6:31 “Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”

Kwahiyo asiwe na wasiwasi hilo suala la baada ya kuiacha hiyo kazi atakula nini? hilo amwachie Mungu.Hivyo mshauri atafute kazi nyingine inayompa Mungu utukufu.  

Ubarikiwe sana.  


Mada zinazoendana:

SADAKA ILIYOKUBALIKA.

TOFAUTI KATIKA YA ZAKA NA SADAKA NI IPI?

NATAKA REHEMA, WALA SI SADAKA!

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

NITAIFAHAMU VIPI KARAMA YANGU?.

IMANI YENYE MATENDO;


Rudi Nyumbani:

 

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/je-mtu-aliyeokoka-anaruhusiwa-kumiliki-guest-house-au-lodge-ambayo-ina-bar-ndani-yake-na-kutoa-fungu-la-kumi-kwa-kupitia-hiyo-kazi/