NABII MUSA.

by Admin | 30 August 2019 08:46 pm08

Musa alizaliwa huko Misri, miaka mingi kidogo baada ya Yusufu mwana wa Yakobo kufariki. Wakati wa kuzaliwa kwake, mama yake alimhifadhi mtoni kutokana na hofu ya amri ya Mfalme juu ya kuuawa kwa wazaliwa wote wa jinsia ya kiume.

Jina la Baba yake Musa ni Amramu na Mama yake ni Yokebedi. (Hesabu 26:59).

Musa alikuwa na Kaka yake wa damu aliyeitwa Haruni waliokuwa wamepishana miaka 3, Haruni alikuwa mkubwa kwa Musa, na ndiye yule aliyekuja kuwa Kuhani Mkuu, pia alikuwa na dada yake aliyeitwa Miriamu ambaye naye pia alikuwa ni Nabii wa Bwana.

Bithiani aliyekuwa Binti wa Farao alimwokota akiwa kwenye kijisafina kidogo, pembezoni mwa mto wakati akiwa anaoga. Musa aliishi katika Nyumba ya kifalme mpaka alipofikisha umri wa miaka 40, Baadaye aliasi nyumba ya Farao kutokana na kumsaidia mmoja wa ndugu zake wa Kiebrania, akakimbilia nchi ya Midiani. Huko alipata mke kutoka kwenye nyumba ya kuhani mmoja wa Midiani aliyeitwa Yethro.

Alikaa miaka 40 nyumbani kwa Yethro, akichunga mifugo yake, mpaka siku moja Bwana alipomtokea katika mwali wa moto, ndani ya kile kijiti, alipokuwa anachunga kundi la Yethro, Alipewa maagizo ya kuwaokoa Israeli waliokuwa wanateswa chini ya utawala mkali wa Farao.

Kwa Ishara nyingi na miujiza mingi Musa aliwaongoza wana wa Israeli miaka 40 mingine, na Alifariki akiwa na miaka 120, akiwa na nguvu zake zote. Macho yake hayakupofuka wala mwili haukupungua nguvu (Kumbukumbu 34:7)

Musa pekee ndiye Nabii aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, wala baada yake hakuinuka nabii mfano wake yeye (Kumbukumbu 34:10-12)

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1.Utaji uliokuwepo juu ya uso wa Musa ulikuwa unaashiria nini?

2.Haruni ni nani?

3. Miriamu ni nani?

HOME

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/30/nabii-musa/