HARUNI

HARUNI

Haruni ni nani

Haruni alizaliwa miaka mitatu kabla ya kuzaliwa Nabii  Musa, alikuwa ni ndugu wa damu kabisa wa Musa. Na walikuwa na dada yao aliyeitwa MIRIAMU. Bwana alimwita Haruni katika huduma baada ya Musa kusita-sita wito wake wa kwenda kwa Farao, na baada ya kutoa vijisababu. Mungu alimwita Haruni ndugu yake awe kama msemaji wake katika safari yao ya kwenda kuwafungua wana wa Israeli dhidi ya mateso ya Farao. (Kutoka 4:10-15).

Haruni pamoja na Musa walikuwa ni wa kabila la LAWI. Bwana aliwapa maagizo kwamba kwa kutumia ile FIMBO wakafanye ajabu zote mbele ya Farao. Fimbo ndiyo iliyokuja kujulikana kama FIMBO YA HARUNI.

Kutokana na utumishi wa Haruni, Bwana alimteua awe KUHANI MKUU, Yeye na wanawe milele. Na kabila la Musa na Haruni, (kabila la Lawi) ndilo lililokabidhiwa shughuli zote za kikuhani, yaani shughuli za kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zote za wana wa Israeli.

Kutokana na upingamizi mkali wa wana wa Israeli dhidi ya uongozi wa Mtumishi wa Mungu, Haruni mara kadhaa alijaribu kuvutwa na ushawishi wao. Na hivyo wakati Fulani kufikia hatua ya kukubali kuwatengenezea sanamu ya ndama (Kutoka 32:1-5).

Haruni naye hakufika nchi ya Ahadi, kutokana na dhambi waliyoitenda wao na Musa ya kujichukulia utukufu mbele ya Wana wa Israeli.(Hesabu 20:10,24) Hivyo alikufa akiwa jangwani akiwa mzee sana.

Ni nini tunaweza kujifunza kutoka kwa maisha ya Haruni? (Haruni ni nani)

Pamoja na mambo mengi yasiyofaa tusiyoweza kujifunza kutoka kwake, kama kuungana na Wana wa Israeli kutengeneza ile sanamu ya ndama… lakini bado Haruni alikuwa ni mtu mwenye ujasiri mwingi kuliko Musa..Wakati Musa anasita sita kwenda kuzungumza na Farao..yeye alichukua nafasi yake kwa kuuvaa ujasiri uliotoka kwa Mungu..

Na jambo lingine la Muhimu ni nafasi ya ukuhani aliyopewa na Mungu..Musa hakupewa nafasi ya ukuhani isipokuwa Haruni na wanawe..Nafasi ya ukuhani inafananishwa na nafasi ya YESU KRISTO, Kama Kuhani Mkuu…Hivyo alisimama kama Kuhani Mkuu wa Mungu kwaajili ya wana wa Israeli. Na Yesu Kristo kama Kuhani mkuu wa wanadamu wote.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

1. Fimbo ya Haruni ilikuwaje?

1.Miriamu ni nani?

2. Musa ni nani?

HOME

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments