Manabii walisema “Neno la Mungu likanijia” ..Maana ya hili neno ni nini?.

by Admin | 31 August 2019 08:46 pm08

JIBU: Kujiliwa na Neno la Mungu ni sawa sawa na kufunuliwa ujumbe unaomuhusu mtu au jamii fulani, na ujumbe huu Mungu anamshushia mtu aidha kwa njia ya ndoto, au maono, au sauti, au kutembelewa na malaika, au njia nyingine yoyote ya ki-Mungu. 

Kwahiyo unaposoma mahali popote kwenye biblia,unakutana na sehemu inasema Neno la Mungu lilimjia Isaya, au Yeremia au Yona, hap ni sawa na kusema, ujumbe utokao kwa Mungu umemfikia Isaya, au Yeremia au Yona awapelekee watu. Kadhalika hata sasa hivi Neno la Mungu, huwa linawajilia watu kwa njia mbalimbali, mt anapofunuliwa Neno lolote kwa njia ya ndoto, au maono au kuzuriwa na malaika, au katika biblia, na Neno hilo limebeba ujumbe wa kwenda kuwapelekea watu wengine, hiyo ni sawa tu na Neno la Mungu limemjia mtu huyo. Kadhalika unaposikia ndani wito wa kwenda kuwashuhudia wengine habari njema, hapo ni sawa na lile Neno linalosema

Marko 16:15 “Enendeni ulimwenguni kote mkahubiri injili kwa kila kiumbe”

limekujia, hivyo unapaswa ukauwasilishe huo ujumbe kwa wakati. Na kuna hatari za kutokutii Neno la Mungu linalokujia, na hatari zenyewe ndio kama zile zilizompata Nabii Yona na zile alizoonywa Nabii Ezekieli zikisema.. 

Ezekieli 3: 17 “Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.

18 Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.

19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.

20 Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako”.

 Ubarikiwe sana.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada zinazoendana:

BIBLIA INASEMA USIONGEZE WALA USIPUNGUZE NENO LA MUNGU, HUKO KUONGEZA NA KUPUNGUZA KUKOJE?

WANA WA MAJOKA.

JIWE LA KUKWAZA

KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.

MADHAIFU.

WITO WA MUNGU


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/08/31/manabii-walisema-neno-la-mungu-likanijia-maana-ya-hili-neno-ni-nini/