by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09
JIBU: Biblia haijaeleza moja kwa moja kuhusu suala la uzazi wa mpango aidha utumike au la, kwasababu njia zinazotumika sasa hazikuwepo katikati ya watu wa kale, Lakini ni vizuri kufahamu lengo la kufanya hivyo ni nini, wapo wengine wanafanya hivyo kwasababu ya matatizo ya kiuchumi, wengine kwasababu ya mapungufu ya kimwili, wengine kwasababu ya kuzuia kuathiriwa kwa kazi yake Fulani, na pia wapo wengine ni kwasababu tu za kiasherati/zinaa n.k..
Hivyo njia nyingi za sasa zitumiwazo kwa uzazi wa mpango zinachukuliwa kwa taswira ya kiasherati kwasababu iko wazi nyingi zinatumiwa hivyo. Lakini ikiwa ni kwa wana ndoa, na dhamira zao zikiwa ni safi mbele za Mungu, na malazi yao ni masafi siku zote, na wanazo sababu za muhimu zinazowalazimu kufanya hivyo labda kwasababu za uleaji wa watoto n.k. Si dhambi wanaweza kutumia. Kwasababu kumbuka pia maandiko yanasema Katika
1Timotheo 5: 8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini”.
Unaona hapo? Uzaaji wa watoto usio na mpango, hususani pale usipokuwa na uwezo wa kuwalea, ni sawa na umeikana Imani. Hivyo ni vizuri kama wewe ni mwanandoa, ukae chini katika maombi na kumuuliza Mungu, na mapatano na mwenzako, na kisha zitumike.
Lakini mambo hayo hayamuhusu mtu asiye mwana-ndoa.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
JE! NI HALALI KUTOA CHETI KWA WAKRISTO WANAOOANA?
JE! KUFANYA MASTURBATION (PUNYETO) NI DHAMBI?
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-ni-halali-kwa-mtu-wa-mungu-kutumia-njia-za-uzazi-wa-mpangoikiwamo-mipira/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.