Je? Ni hatua zipi muhimu za kufuata baada ya kubatizwa?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Kwanza, ni vizuri kufahamu kubatizwa, ni tendo la rohoni, na linapaswa litoke rohoni, kitendo cha mtu kwenda kubatizwa kwanza anapaswa awe tayari kugeuka [kutubu], kwa kumaanisha kabisa kutoka moyoni mwake, kuacha maisha ya dhambi, na kuanza maisha mapya katika Kristo…

Sasa mtu wa namna hiyo BWANA YESU KRISTO akishaona moyo wake kweli umedhamiria kugeuka, na hajafanya hivyo kama ni desturi za kidini tu ili kutimiza wajibu, sasa moja kwa moja mtu wa namna hiyo anapewa UWEZO WA KUSHINDA dhambi, kwasababu yeye mwenyewe hawezi. soma

Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea ALIWAPA UWEZO wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”

Sasa Uwezo huo hauji juu ya mtu kama hajadhamiria kabisa kuacha dhambi zake, ikiwa na maana kudhamiria kuacha ulevi, anasa, uasherati, utukanaji, uongo, wizi na mambo yote yanayofanana na hayo..

Hivyo kitendo cha Kubatizwa kama mtu akizingatia vigezo hivyo, ubatizo ule unakuwa na maana kubwa sana katika maisha yake kuanzia huo wakati na kuendelea, yeye anakuwa ni milki halali ya Kristo YESU. Ile hatia ya dhambi Bwana anaifuta juu yake, na UWEZO wa kushinda dhambi unaachiliwa juu yake..Kwahiyo, kitu anachopaswa kufanya sasa kuanzia huo wakati wa kubatizwa na kuendelea, ni KUTOKUMZIMISHA ROHO WA MUNGU NDANI YAKE….Na hii inakuja kwa kudumu katika usafi wa roho, na kujifunza Neno la Mungu, na kukaa karibu na ndugu wa kikristo wenye Imani moja na wewe.

Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?

JE, KAMA HAUNA UBATIZO SAHIHI HAUWEZI KUWA NA ROHO MTAKATIFU?

WALIO NA HEKIMA NDIO WATAKAOELEWA.

ROHO I RADHI, LAKINI MWILI NI DHAIFU.

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?

CHANZO CHA MAMBO.


 

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-ni-hatua-zipi-muhimu-za-kufuata-baada-ya-kubatizwa/