Je! ni sahihi kwa Mkristo kusherekea siku yake ya kuzaliwa.[Birth day]?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

JIBU: Sherehe yoyote ile iwe ni ya kuzaliwa, au mahafali, maadhimisho ya miaka ya ndoa, harusi, kumbukumbu n.k. Biblia haitatoa katazo lolote kufanyika, isipokuwa imetoa katazo tu kwa KARAMU ZA ULAFI.

Tukisema karamu za ulafi tunamaanisha karamu/sherehe zozote zinazovuka mipaka ya Neno la Mungu, kwamfano sherehe zinazochanganyikana na pombe,Disco, miziki ya kidunia, uvaaji mbovu, na mambo yote yafananayo na hayo ambayo ni kunyume na Neno la Mungu, hizo zote ni karamu za ULAFI ambazo biblia imezikataza. Ukisoma..  

1Petro 4: 3 “Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na KARAMU ZA ULAFI, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;”  

Unaona hapo pia ukisoma …  

2 Petro 2: 13 “Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu WAKIFUATA ANASA ZISIZO KIASI KATIKA KARAMU ZAO ZA UPENDO, wafanyapo karamu pamoja nanyi; ”

  Unaona pia hapo karamu/sherehe zenye mambo kama hayo ndani yake ni dhambi kwa mkristo kufanya, lakini ikiwa ni kwa ajili ya kuhitimu, au kuzaliwa, au ndoa, au mahadhimisho unaweza ukasheherekea upendavyo lakini hapo ndio kuzingatia lile neno linalosema Wakolosai 3: 17 “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.  

Na ndio maana Bwana YESU alitushauri pale tunapojisikia kufanya karamu au kusheherekea kwa namna yoyote ile tufanye kwa manufaa ya kimbinguni zaidi, yaani kuliko kuwaalika watu wenye cheo, ni vizuri kusheherekea na watu maskini, ili thawabu yetu iwe kubwa mbinguni (Luka 4:12)..Kuliko kukata keki na ndugu zetu au na marafiki zetu tu, ni vema tukaongeza pia kukata na yatima waliokaribu nasi pamoja na wajane.. Ndio karamu yenye harufu nzuri mbele za Mungu.

  Ubarikiwe.


Mada zinazoendana:

JE! SISI KAMA WAKRISTO NI DHAMBI KUSHEHEREKEA KRISMASI?.

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUOA/KUOLEWA NA MTU WA IMANI NYINGINE?

NI SAHIHI KUMUITA MARIAMU, MAMA WA MUNGU?

JE! NI SAHIHI KWA MKRISTO KUNING’INIZA PICHA NYUMBANI MWAKO KAMA YA YESU?

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

KARAMA ILIYO KUU.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/je-ni-sahihi-kwa-mkristo-kusherekea-siku-yake-ya-kuzaliwa-birth-day/