Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno;” maana yake nini?

by Admin | 1 September 2019 08:46 pm09

SWALI: Nini maana ya huu mstari? “Mathayo 13:30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu. ”


JIBU: Mfano huu Bwana alioutoa unahusu siku za mwisho, na kumbuka siku za mwisho ndio hizi tunazoishi sasa mimi na wewe, kwamba Bwana atatuma wavunaji watakaovuna watu, sasa ili kuelewa hawa wavunaji ni wakina nani hebu tusome mstari ufuatao..

Mathayo 9:37 “ Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.”

Unaona hapo, siku hizi za mwisho, wahubiri ndio wavunaji, na siku hizi za mwisho Bwana amesema atawatuma wengi,wa ukweli na wauongo, ambao watawavuna watu wote walioko ulimwenguni (waovu na wema), wale walio waovu (wanaofananishwa na magugu) watafungwa matita matita (yaani watafungwa katika madhehebu mbali mbali) na watasubiria kutupwa katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti, kwasababu ni magugu.

Kama unapenda uasherati, utapata muhubiri atakayekufariji katika uasherati wako, vivyo hivyo na mambo mengine maovu, utapata wahubiri na waalimu na makanisa yanayochukuliana na hayo mambo.

Lakini wale walio wema(yaani zile ngano njema) zitakusanywa pamoja na kuhifadhiwa ghalani (na ghalani ni mbinguni), wale walio tayari kufumbua macho yao waone, kufumbua masikio yao wasikie, Bwana anawakusanya katika siku hizi za mwisho kupitia wahubiri wake waaminifu na wa kweli na kuwaweka tayari kwa ajili ya unyakuo.

Je! Na wewe umejiandaaje? Huu ni wakati wa kukusanywa,Unakusanywa wapi leo? Kwenye dhehebu lako? au katika Neno la Mungu?.

Kanisa/muhubiri asiyekuhubiria kwamba Ibada za sanamu,ulevi,ulavi,ulawiti,uongo,rushwa,wizi,masturbation, chuki,usengenyaji,uvaaji vibaya, ni tiketi ya kwenda motoni, basi huyo ni mvunaji ametumwa kukufunga katika tita lake, na kukupeleka motoni, Biblia inasema mtu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni na pasipo huo UTAKATIFU hakuna mtu atakayemwona Mungu.

Ubarikiwe!

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

HUIJUI KAZI YA MUNGU, AFANYAYE MAMBO YOTE.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA.

LULU YA THAMANI.

MSHIKE SANA ELIMU.

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

TUZIJARIBU HIZI ROHO.


Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/01/viacheni-vyote-vikue-hata-wakati-wa-mavuno-2/