by Admin | 2 September 2019 08:46 pm09
SWALI: 2 Samweli1:17-18. Inasema: Daudi akamwomboleza Sauli,na Yonathani, mwanawe,…”(Kama ilivyoandikwa katika KITABU CHA YASHARI’).Hicho kitabu cha Yashari ni kipi?
JIBU: Kumbuka Biblia sio kitabu cha kinabii tu kutabiri mambo yajayo peke yake, hapana bali pia ni kitabu kilichorekodi historia ya mambo yaliyopita, Na hiyo yote ni ili kutufundisha na kutuonya sisi kwa mifano iliyo hai ambayo ilishawahi kutokea huko nyuma,tuamini na kugeuka,
Hivyo sikuzote ili historia iweze kukubalika kuwa ni kweli ipo wazi kuwa ni lazima iwe imetibitishwa kwa ushahidi zaidi ya mmoja, Kwa mfano haiwezekani historia ya vita vya Kagera ijulikane na watanzania tu peke yao watu wengine duniani wasiifahamu, yaani tujitangaze duniani kote sisi tulipigana vita na Uganda, lakini hakuna taifa hata moja lililoona hilo na kuthibitisha habari hiyo, kwa namna moja au nyingine zinaweza zikawa ni habari za kuzusha tu, lakini kama jirani zetu wakenya walishuhudia ni kweli, waganda walishuhudia ni kweli tulipigana nao, na Waafrika wote waliokuwepo kipindi kile watashuhudia jinsi walivyoshirikiana na sisi katika vita vile, basi hiyo vita kwa asilimia zote itakuwa ni ya ukweli na ilishawahi kupiganwa na hata kwa vizazi 100 vijavyo havitaweza kukana kwa ushahidi huo.
Vivyo hivyo biblia nayo, ilivyoandika habari, kwa kuwathibitishia watu kuwa hayo yote ni kweli ikiwa kama mtu atatokea hatoamini kilichoandikwa, basi vipo vitabu vingine ambavyo vimerekodi habari za matukio hayo hayo biblia iliyoyarekodi, na mojawapo ndio hichi kitabu cha YASHARI ambacho tunaona kimeandika maombolezo ya mashujaa na sehemu nyingine matendo makuu yaliyofanywa na mashujaa wa Israeli. Sasa tafsiri ya hilo Neno Yashari “NI MTU MWEMA AU MTU MTU WA HAKI”, hili ni Neno la Kiyahudi, hivyo kitabu cha Yashari ni kitabu cha mtu mwema, au mtu wa haki, na kitabu hichi katika biblia hakijazungumziwa hapa tu tunakisoma pia katika kitabu cha Yoshua :
Yoshua 10:12 “Ndipo Yoshua akanena na Bwana katika siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.
13 Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo, Je! Hayakuandikwa ndani ya kitabu cha YASHARI? Basi jua likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanya haraka kuchwa kama muda wa siku nzima”.
Unaona, vipo pia vitabu vingine vinatajwa mbali na hii biblia yetu, ukisoma Hesabu 21:14, utaona kimoja kinaitwa kitabu cha VITA VYA BWANA. Ukisoma pia (1Nyakati 29:29), Utaona kulikuwa na kitabu kinachojulikana kama KITABU CHA TAREHE CHA SAMWELI MWONAJI, kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Nathani nabii, na pia kulikuwa na kitabu cha tarehe ya Gadi mwonaji; Pia kulikuwa na kitabu cha tarehe cha wafalme wa Yuda, ukisoma (1Wafalme 14:29), utaliona hilo:..
1Wafalme 14:29 “Na mambo yake Rehoboamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?”
Unaona vyote hivyo vilinakili matukio ambayo biblia ilirekodi pia. Lakini sasa hiyo haimaanishi kuwa ni vitabu vilivyovuviwa na Roho Mtakatifu kwamba vitumike kuwa mbadala wa Biblia hapana, Hivyo vipo kuithitisha kuwa Biblia ni kweli na sio biblia kuthibitisha kuwa vitabu hivyo ni kweli. Halikadhalika leo hii, utasema mimi siiamini kuwa biblia ina habari za ukweli, wala siamini kama YESU alizaliwa na bikiria kwa uweza wa Roho Mtakatifu, wala siamini kama alipaa, hizo ni hadithi za kutunga tu, zilibuniwa tu na watu Fulani Rumi, lakini nataka nikuambie vipo vitabu vingi vya historia na vya kidini mbali na hiyo biblia unayoitilia mashaka na vyote vinathibitisha ujio wa kwanza wa Yesu Kristo kuwa ni yeye pekee ndiye aliyezaliwa na bikiria kadhalika vinathibitisha ujio wake wa pili duniani kuwa atakuja kuuhukumu ulimwengu wote. na mojawapo wa vitabu hivyo ni QURAN!..
Sasa sio kwamba Qurani ni kitabu cha kweli cha Mungu hapana, kina mambo mengi sana yasiyo ya ukweli, lakini ndani yake kibebea chembechembe ndogo za ukweli kwamba ni kweli alishawahi kutokea Mtu wa kipekee aliyezaliwa bila dhambi na kuishi duniani anayeitwa YESU, na huyo atarudi tena mara ya Pili. JE! Mambo yote Yesu aliyoyafanya tangu kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake, na kurudi kwake hayakuandikwa katika kitabu cha waislamu Quran?. Ni uthitisho gani tena unahitaji? Utakwenda wapi uukimbie uso wa Mungu, na ukweli uliopo katika Kristo Yesu?. Tubu leo YESU ndiye Njia kweli na uzima, NA YUPO MLANGONI KURUDI TENA, Hakuna tumaini nje ya yeye. Wala siku ile hakutakuwa na cha kujitetea.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?
VITABU VYA BIBLIA: SEHEMU YA 1
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)
SHETANI ANATOLEA WAPI FEDHA, ANGALI TUNAJUA FEDHA NA DHAHABU NI MALI YA BWANA?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/09/02/kitabu-cha-yashari-kinachozungumziwa-katika-2samweli-117-18-ni-kitabu-gani/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.