JIBU: Uumbaji wa Mungu umegawanyika katika sehemu kuu mbili…
Sehemu ya kwanza: Ni Viumbe vya kimbinguni …Viumbe hawa wa kimbinguni nao wamegawanyika katika sehemu kuu mbili, nao ni malaika na wanadamu…Malaika wanaishi mbinguni, na wanadamu wanaishi duniani…Ingawa asili yao wote ni mbinguni..Ndio maana kuna usemi usemao sisi ni wasafiri tu, ulimwenguni sio kwetu..(Waebrania 11:13-15 na 1Petro 2:11), Wanadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu na sura ya Mungu,
Kwa kawaida hata mtu akiwa na sura inayofanana sana na yako, ni dhahiri kuwa huyo anaweza kuwa mwanafamilia au mwenye tabia zinazoendana sana na wewe…Na kama ni mwanafamilia basi lolote litakalotokea aidha kifo, au sherehe, au chochote kile ni lazima familia yako ihusike,..Na sisi wanadamu kwasababu tunafanana na Mungu basi ni familia ya Mungu na hivyo tukifa tunamrudia Baba mkuu wa familia yetu, aliyetuzaa yaani Mungu. Uwe mwovu uwe mwema, hilo haliepukiki maadamu una umbo na sura ya mwanadamu…tayari asili yako ni kwa Mungu.
Na sehemu ya Pili ya uumbaji wa Mungu ni viumbe vya kidunia, ndio Wanyama, samaki, ndege, miti, hivi vyote navyo vina uhai. Lakini hivi havijaumbwa kwa mfano wa Mungu, Mungu hafanani na Wanyama…Mungu hana mkia kama simba wala hana pembe, wala hana matawi na mizizi kama miti ilivyo…
Hivi vimeumbwa kutoka katika ardhi soma (Mwanzo 1:12 na 1:24), hivyo familia yao ni katika ardhi…na vikifa haviendi popote Zaidi ya ardhini..kwasababu duniani ndio kwao…Vimeumbiwa udunia, havina mahali pa kwenda baada ya hapa…Ndio maana havijui kama kuna kitu kinachoitwa Kesho, wala havitafakari mwaka jana kulitokea nini na Kesho kutatokea nini, na wala havitafakari vipo wapi, hiyo ni kwasababu havisafiri vipo nyumbani kwao ambapo ndipo hapa duniani. Na kwasababu nyumbani kwao ni hapa duniani na vimetolewa kutoka katika ardhi kama biblia inavyosema basi vikifa habari yao ndio imeishia hapa hapa…Mnyama akifa habari yake ndio imeishia hapa hapa, hawana ufufuo, mti ukifa habari yake ndio imeishia hapo hapo, hakuna ufufuo, bakteria akifa habari yake ndio imeishia hapo hapo hakuna ufufuo na viumbe vingine vyote tofauti na wanadamu.
Lakini mtu akifa roho yake inamrudia Muumba wake aliyeko mbinguni, kwa Baba wa familia yake. Na kuhukumiwa na yeye, ikiwa amestahili uzima basi ataishi milele, akiwa hajastahili basi anaangamizwa milele,.