by Admin | 2 October 2019 08:46 pm10
Maana ya kanisa ni “walioitwa” kwahiyo watu walioitwa watoke sehemu fulani wanaitwa kanisa…..Hivyo tafsiri ya kanisa sio jengo kama inavyodhaniwa na wengi…
Kwahiyo katika maandiko kanisa la kwanza lilianza siku ile ya PENTEKOSTE. Roho Mtakatifu aliposhuka juu ya watu! Soma Matendo Mlango wa pili yote.
Wale waliomwamini Yesu, na kubatizwa walishukiwa na Roho Mtakatifu, na hivyo Roho huyo huyo aliwaongoza kukusanyika pamoja kwa lengo la kujifunza Neno ambalo Mitume ndio waliokuwa wanalifundisha, pia walidumu katika kushiriki meza ya Bwana, katika kufanya ushirika na katika Kusali. Hayo mambo manne ndiyo yaliyokuwa yanafanyika katika kanisa la kwanza.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali”.
(Hilo ndilo kanisa la kwanza)
Kanisa katoliki llinalosemekana kama kanisa la kwanza, hilo ilikuja kuzaliwa mwaka wa 325 Baada ya Kristo. Ambalo hilo lilikuwa kinyume na kanisa la kweli la Kwanza la Pentekoste.
Kanisa katoliki, ni kanisa la uongo kwasababu halikudumu katika hayo mambo manne hapo juu… halidumu katika fundisho la Mitume kama kanisa la Kwanza, fundisho la Mitume linasema tusiabudu sanamu na pia linasema mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja tu Yesu Kristo, wakati kanisa katoliki linaamini Mariamu pia ni mpatanishi…..
Pia kanisa katoliki halidumu katika kumega mkate, kwani mwenye ruhusu ya kushiriki ni Padre tu! peke yake jambo ambalo ni kinyume na maandiko, pia halidumu katika kufanya ushirika wala kusali…Sala zinazofanywa ni za desturi za kipagani, kusalia rozari na sanamu jambo ambalo kanisa la kwanza halikufanya. Maombi ya moja kwa moja kwa Mungu hayatiliwi mkazo, na zaidi ya yote maombi ya masafa marefu hayapo kabisa ndani ya kanisa katoliki.
Mada Nyinginezo:
JE! BIKIRA MARIA NI MALKIA WA MBINGUNI?
JE! NI SAHIHI KUMUITA MARIA MAMA WA MUNGU?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/02/kanisa-la-kwanza-duniani-ni-lipi/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.