by Admin | 22 Oktoba 2019 08:46 um10
Waefeso 5.12 “kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena”.
Zamani ilikuwa ni rahisi kumtambua mtu mwenye dhambi kwa kumtazama tu au kumwangalia mienendo yake kwasababu karibu kila ouvu uliokuwa unafanyika chanzo chake kilikuwa ni cha nje kabisa kinachoonekana,kwamfano zamani ilikuwa ili kuwapata watu wanaotembea tupu au makahaba ilikuwa ni lazima uende mahali kama kasino, au disco za usiku, au kwenye madanguro lakini sasahivi mambo hayo yote unayapata mitandaoni na kwenye simu za mikononi bure, maovu yanayotendeka sasahivi kwa siri ni mabaya zaidi kuliko hata yale ya kipindi kile,..mtu anaweza akatembelea madanguro hata 30 katika simu yake katika siku moja.
Unaweza ukajifanya mwema kwa nje, haunywi pombe, hauendi disco, hauzini na wanawake, au wanaume, tena umebatizwa, na unasema wewe ni mkristo, lakini ndani ya simu yako kwa siri siri ume download video za pornography unatazama na hakuna mtu anayejua, nataka nikuambie biblia inasema hilo nalo litafika hukumuni siku ile..
Mhubiri 12:14 “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja NA KILA NENO LA SIRI, likiwa jema au likiwa baya
Wala usijidanganye, kusema mengine yote nimeyashinda ni hili tu ndio linalonisumbua siku ile Mungu atanihurumia, ndugu kuzimu utakwenda, biblia inasema
Yakobo 2:10 “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote”.
Kila unapoingia mtandaoni kazi yako ni kutafuta picha na video za watu wa kidunia wanaozini, kila update ya video za ngono wewe unayo, Kumbuka Moja ya vitu sita ambavyo Mungu anavichukia ni pamoja na mtu aliye na miguu myepesi kukimbilia maovu..(Mithali 6:18)
Wewe hujui ni kwa namna gani unamkasirisha Mungu, Badala uwe mwepesi kutafuta maneno yake mitandaoni wewe unatumia wepesi huo kwenda kutafuta miziki ya kidunia ambayo maudhui yake ni uasherati tu, na matusi, ni kibaya zaidi unajiita mkristo.
Hujui kuwa unatimiza maandiko ya wale wakristo baridi wanaozungumziwa kuwepo katika siku za mwisho, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu.(2Timotheo 3:4 )
Ni heri ukaitupilia mbali hiyo simu kama inakukosesha kuliko kuwa mtumwa wa ibilisi na ukaenda kuzimu, biblia inasema kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate….wapo watu wengi kuzimu leo hii, wanatamani wakuhubirie wewe injili, uache kutazama hayo mambo machafu unayoyotazama huko mitandaoni, lakini hawawezi kutoka huko, laiti ungewaona, wanavyohangaika na ule moto kwa kosa moja kama unalolifanya wewe leo hii, usingetamani hata kutazama pornography, fahamu kuwa asilimia 99 kama sio 100, ya watu wote wanaoigiza mikanda hiyo ni ma-agents wa kuzimu, tena wale wa hali ya juu sana, wanapokea maagizo hayo kuotka kwa ibilisi mwenyewe baba yao, na wanaelekezwa namna ya kufanya mambo hayo, sasa wewe usiyejua unavutiwa kwenda kutazama, hujui kuwa kuna maroho mabaya yenye nguvu mara 7 zaidi ya yale yaliyokuwepo Sodoma na Gomora, yametegeshwa pale, unapotazama tu kidogo, moja kwa moja, yanakuvaa na ndio hapo tamaa zisizo za kawaida zinakuvaa, zinakufanya uwe kama mnyama aliyerukwa na akili asiyeona aibu kujafanya jambo lolote lile, na hizo hazitoki leo wala kesho, ndio hao wengine wanaishia kuwa mashoga na wasagaji, wengine wanazini na wanyama, wengine na wazazi wao, wengine na watoto wao, wengine ndugu zao, wengine na majirani zao, wengine wanafanya mustarbation… sasa hizo zote ni roho za mauti, ambazo mwisho wake ni kuzimu na hizo roho huwezi kuzishinda kama utaendelea kuwa mbali na Kristo..
Lakini ukidhamiria kabisa kuacha na kutubu dhambi zako, Kristo atakuvika uwezo wa kuvishinda hivyo vyote, Wengi hawawezi na wamekuwa watumwa wa hayo mambo ni kwasababu hawajadhamiria kwa miguu yao yote kumfuata Kristo, moyoni mwake anasema nikimfuata YESU inamaanisha sitakunywa pombe tena, sitatukana tena, sitakwenda disco tena, sasa watu wa namna hiyo hata kama leo hii wakitubu na kusema wamemkabidhi YESU maisha yao, na huku wanavitamani bado vitu hivyo, hawawezi kuvikwa huo uwezo utokao juu wa kuyashinda hayo yote, hata wafanye nini lakini ukidhamiria kwa dhati na kusema, kuanzia leo dunia bye! Bye!
Mimi kwa miguu yote naenda kwa Kristo bila kugeuka nyuma, kwasababu nataka niende mbinguni, nakuambia wewe mwenyewe utaona jinsi itakavyokuwa rahisi kuishinda dhambi, hata sisi tulikuwa huko, tukatolewa ile kiu ya pombe Yesu ataimaliza yote, ile kiu ya sigara itamalizwa yote, ile tamaa ya uzinzi Mungu ataiua, ile tamaa ya kufanya punyeto, itakufa yote, ile tamaa ya ushoga na usagaji itakufa yenyewe..Lakini sharti kwanza useme nimeamua kwa moyo wangu wote, na akili zangu zote, na nguvu zangu zote kuanzia leo kumfuata Kristo. Ukafuta video zote ulizozidownload, ukaacha kutembelea website zote ngono unazozitembelea, ukafuta miziki yote ya kidunia, na ukakaa mbali na wazinzi wote, basi Mungu atakubadilisha haraka sana.
Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba.. “Mungu hawezi kutupa maagizo ambayo anajua sisi hatuwezi kuyafanya”…
Hawezi kutuambia tusizini na huku anajua hatuwezi kuishi bila kufanya uzinzi, kwahiyo anajua kabisa kuna namna mwanadamu anaweza kuishi bila kuzini kabisa! Ipo namna! Na ni rahisi sana…anajua hilo, hivyo ni jukumu letu kuivumbua hiyo, na Hiyo namna ipo kwa Yesu tu mwanawe mpendwa basi!! Ukivifuta hivyo vitu na kuviacha yeye si mwongo kutupa mzigo tusioweza kuubeba…utashangaa tu! Uwezo wa ajabu umekuja juu yako unaokufanya usitamani tena huo uchafu milele!
Kama ni hivyo, na unataka kumkabidhi Bwana YESU maisha yako tena, basi sala ya toba ni hii : hapo ulipo Piga magoti, kisha chukua muda mchache mweleze Mungu kuwa ulimkosea, kwa kuwa vuguvugu, na kutenda dhambi nyingi kwa siri, mwelezo bila kumficha chochote kwasababu mambo yote uliyokuwa unayafanya kwa siri yote anayajua, hivyo mweleze kuwa hutaki kufanya hivyo tena, na kwamba umedhamiria kuacha maisha ya kidunia na sasa unamfuata Kristo..
Ukishasema hivyo kwa kumaanisha kabisa..Ujue kuwa Bwana YESU amekusikia,..baada ya sala hiyo, ni kufuta sasa hivi bila kuangalia kushoto wala kulia kila picha, mziki, video chafu yoyote uliyonayo kwenye simu, flash, laptop au popote pale na Hatua inayofuata ni kutafuta kanisa la kiroho wanalobatiza ubatizo sahihi wa maji mengi kwa jina la YESU KRISTO nenda ukabatizwe kwa ajili ya kukamilisha wokovu wako, kulingana na Matendo 2:38, Kisha Mungu atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu bure atakayekuwa msaidizi wako, kukufundisha na kukuongoza kulielewa Neno na kuishi Maisha ya utakatifu…Vile vile usiache kwenda kanisani kuanzia leo ili Mungu ayakamilishe maisha yao mpaka siku ile ya wokovu.
Bwana akubariki sana. Ikiwa utapenda kuendelea kujifunza Neno la Mungu pamoja na sisi ya kukua kiroho, basi usiache kutembelea website yetu hii (www wingulamashahidi org).
Maran Atha!
Mada Nyinginezo:
KWANINI MAHUSIANO YA JINSIA MOJA NI DHAMBI?
JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.
DALILI NYINGINE INAYOUTAMBULISHA UZAO WA NYOKA.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/22/kuwa-makini-na-mitandao-ni-shimo-refu/
Copyright ©2023 WINGU LA MASHAHIDI WA KRISTO unless otherwise noted.