BARAGUMU NI NINI?

by Admin | 26 Oktoba 2019 08:46 um10

Baragumu ni nini/ Nini maana ya Baragumu.

Baragumu kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni “Tarumbeta” au “Parapanda” au Mbiu!..Matarumbeta au Mabaragumu yalikuwepo ya aina nyingi kulingana na Nyakati.

Nyakati za zamani mabaragumu yalikuwa yanatengenezwa kwa pembe za wanyama, Tofauti na nyakati zetu hizi Mabaragumu yanatengenezwa kwa shaba na wakati mwingine chuma.

Katika nyakati za zamani Mabaragumu yalitumika katika nyimbo,  hata sasa yanatumika katika Nyimbo, Katika maandiko tunasoma Daudi alisema kwa uweza wa Roho..

Zaburi 150:3 “Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;”

Na Baragumu lilitumika pia kuashiria Mwanzo wa Jambo fulani au mwisho wa Jambo fulani..Kwamfano katika biblia Wana wa Israeli wana wa Israeli walipokwenda vitani, Baragumu ndio iliyokuwa inatambulisha mwanzo wa vita au mwisho wa vita.

Na katika kitabu cha Ufunuo pia Mlango wa 8, Tunaona malaika wakiwa na Baragumu saba, kutangaza mambo yatakayokwenda kutokea kipindi kifupi kijacho

Ufunuo 8:1 “Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa.

2 Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba”.

Je! na kwetu sisi wakristo Baragumu ni nini?.

Kadhalika Pia sisi wakristo hivi karibuni Baragumu moja la Mwisho litapigwa kwetu, baragumu(tarumbeta) hilo ni parapanda ya mwisho ambayo watakatifu wote waliooshwa kwa damu ya Mwana kondoo watanyakuliwa juu na kwenda kuonana na Bwana juu mbinguni. Baragumu hilo halijatengenezwa kwa pembe za wanyama wala shaba! bali kwa malighafi ya kimbinguni. Sauti ya Baragumu hilo itapenya mpaka kwa wafu na wataisikia sauti yake na kutoka makaburini.

Siku hiyo itakuwa ni siku ya shangwe na furaha isiyo na kifani, lakini pia itakuwa ni huzuni kwa walioachwa. Ni wajibu wetu kujitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba..

Bwana akubariki.


Mada Nyinginezo:

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

NI KWANINI MUNGU HAONEKANI?

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

BWANA ALIPOSEMA “SIKUJA KUTANGUA TORATI BALI KUITIMILIZA” ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?

KATIKA 1YOHANA 5:6-9, (A) NI KWA NAMNA GANI YESU ALIKUJA KWA MAJI NA DAMU?

KATIKA MARKO 2:2-12, KWANINI BWANA YESU ALICHUKUA HATUA YA KUSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE KIWETE?


Rudi Nyumbani:

WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/10/26/baragumu-ni-nini/