KUOTA UMEPOTEA.

by Admin | 4 November 2019 08:46 pm11

Kuota umepotea mjini, au kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua, kwa vyovyote vile maadamu ni ndoto ya kupotea basi fahamu kuwa ndoto za namna hii mara nyingi zinatokana na Mungu.

Na huwa zinakuja kwa makundi yote ya watu, (Yaani wale walio ndani ya Kristo na wale walio nje ya Kristo).

Sasa ikiwa kama wewe hujaokoka  Biblia inasema:

Zaburi 37: 18 Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele. 

19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. 

20 Bali WASIO HAKI WATAPOTEA, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.

Unaona wasio haki sikuzote huwa wanapotea, hivyo  kuota umepotea ni ujumbe ambao Mungu anakuonyesha hali yako ilivyo rohoni, na kama vile huko ndotoni unavyojiona unahangaika huku na kule kutafuta njia sahihi ya kufika mahali unapotaka kufika na unashindwa, unateseka sana huku na kule, unaonyeshwa kuwa kuna wakati utafika utautafuta huo wokovu ulioupoteza na hautauona milele…na kibaya zaidi wakati huo utakuwa umeshachelewa.

Zaburi 1:6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.

Mungu anakupenda na ndio maana anakuonyesha mambo kama hayo mapema ili utengeneze njia zako sasahivi, maadamu upo hai, maadamu imeitwa leo, Kesho inaweza isiwe yako, unaweza ukajiona upo sawa sasa katika Maisha yako, labda umejiendeleza, umefika mbali, una afya nzuri, umefanikiwa, unayo familia nzuri, lakini Mungu anakuambia umepotea, haijalishi upo katika mafanikio gani leo hii, Unachopasw kufanya ni ugeuke uombe msaada kwa Mungu naye atakuonyesha njia…na njia yenyewe ni YESU KRISTO.

Yohana 14:6  “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.  

Unaona kama yeye ni njia basi alikuja kukitafuta kilichopotea kama anavyosema katika..

Mathayo 18:10  “Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

11  [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea”.]

Kwahiyo ikiwa leo utakubali kutii na kumpa Maisha yako, basi atayaokoa na kukusamehe kabisa, ikiwa upo tayari sasa, hapo ulipo piga magoti kisha chukua dakika chache tafakari mambo yote maovu ulioyomfanyia Mungu, kisha kwa Imani, zungumza na Mungu, mwombe rehema,usimfiche chochote mwambie akusamehe maanisha kabisa kwasababu hapo ulipo anakusikia…Kisha ikiwa toba yako imetoka moyoni kwa dhati, na kwamba upo tayari kuacha yote ya nyuma uliyoyafanya basi fahamu kuwa Mungu amekusamehe, hivyo tu,

Sasa hatua inayofuata ni kwenda kutafuta mahali wanapobatiza

Ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO sawasawa na (Matendo 2:38) Ili ukamilishe wokovu wako uwe milki halali ya YESU KRISTO, ndipo Mungu akumwagie kipawa chake cha Roho Mtakatifu. Hivyo zingatia hayo maagizo yote ni muhimu sana kuyafanya, ikiwa hufahamu vizuri ni wapi utapata ubatizo sahihi, basi wasiliana na sisi kwa namba hizi 0789001312 au 0654555788.Tutakusaidia kutafuta maeneo karibu na wewe.

Vile vile ikiwa wewe tayari ulishaokoka, na ndoto kama hizi, kuota umepotea shuleni, au kuota umepotea msituni, au kuota umepotea njia panda au kuota umepotea katika riadha au kuota umepotea sehemu usiyoijua zinakujia, basi fahamu kuwa Mungu anakukumbusha kuwa, unakaribia kuiacha njia ya wokovu, aidha kuna uamuzi unaokwenda kuufanya ambao utakupotezea ramani yako ya wokovu moja kwa moja, au umeshaanza kuifanya..au kuna dhambi unaitenda ambayo haimpendezi Mungu sasahivi,Hivyo kuwa makini sana.. Shika sana ulicho nacho asiye mwovu akalitwaa taji lako.

Ezekieli 44: 9 Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli. 

10 Lakini Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe.

Kwahiyo jitazame, kumbuka Bwana alipokutoa, usimwache yeye..Mungu anakuonya kwa njia hiyo kwasababu anakupenda..Hivyo ukiona unalolijfanya sasahivi linakutenga na Mungu kama linakushinda nguvu ya kulitawala  basi liweke kando mtafute muumba wako kwanza kwa usalama wa roho yako na hayo mengine yawe baadaye kama yatakuwa na umuhimu.

Ubarikiwe sana.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

NYOTA ZIPOTEAZO.

KUOTA UPO UCHI.

Kuota unafanya Mtihani.

KUOTA UNA MIMBA.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/11/04/kuota-umepotea/