Kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate.

by Admin | 7 December 2019 08:46 am12

Bwana Yesu alikuwa na maana gani aliposema “kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate”?


JIBU: Sentensi hiyo ina tafsiri mbili..Tafsiri ya kwanza ni ya rohoni, na pili ni ya mwilini…Tukianza na tafsiri ya rohoni ambayo inamaanisha viungo vyote vya rohoni. ..Kwamba kitu chochote kile ambacho ni kikwazo cha sisi kuingia mbinguni hicho ni sawa na kiungo, Umaarufu unaweza kuwa ni kiungo,.. marafiki wakati mwingine wanaweza kuwa ni kiungo (kwasababu wapo marafiki ambao ukikaa nao unaweza kuikosa mbingu, hivyo ni wakukata ili kuinusuru roho yako)..Shughuli ni kiungo (Zipo shughuli au kazi ambazo ukizifanya zitakukosesha mbingu haijalishi zimehalalishwa na nchi kiasi gani)..n.k

Tafsiri ya pili na ya muhimu inahusu viungo vya mwili. Mkono unaweza kukukosesha kuiona mbingu., kama mkono wako umezoea wizi., kila ukipita unatamani kudokoa, kama mkono wako umezoea kufanya masturbation, ..Kama imeshindikana kuamua kuacha kufanya hayo mambo kwa njia ya kawaida basi ni bora uukate huo mkono…ili usije ukakupeleka jehanamu ya moto… Kadhalika na ulimi wako kama unakusababisha kila dakika uzungumze mambo ya watu wengine vibaya, au uchonganishe au utukane ni heri ukaukata ili ujiokoe na ziwa la moto…

Biblia inasema…

Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.

10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo”.

Sasa hata mambo mawili yakiwekwa mbele yangu, nikaambiwa nichague moja,..kwamba ulimi wangu ukatwe niingie mbinguni au nibaki na ulimi wangu niingie Jehanamu…Ukweli ni kwamba nitachagua kukatwa ulimi ili niingie tu mbinguni Na kila mtu ni wazi atachagua hivyo hivyo.

Na viungo vingine vyote ni hivyo hivyo..kama vinatukosesha tumepewa ruhusa ya kuviondoa..sio dhambi! ..Kama tu tunaweza kuondoa figo iliyo na kansa mwilini, ili tu mwili wote usije ukafa…kwanini tushindwe kukata kiungo kimoja ambacho tusipokitoa kitatugharimu ziwa la moto?..Kama unaweza kufanyiwa operation ya kukatwa miguu ili ugonjwa usisambae mwili mzima au kukatwa ziwa ili tu kansa isikumalize mwili wote..kwanini tushindwe kuondoa hivyo hivyo kama vinakuwa sababu ya kutupeleka jehanamu…?

kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate.

Wengi wanapenda kulipooza hili Neno la Bwana Yesu na kusema kwamba “hakumaanisha viungo vya mwilini”..Alimaanisha viungo vya mwilini na vya rohoni..vyote viwili!!..Ni kweli tunavipenda viungo vyetu lakini kama vinakuwa ni vikwazo vya kwenda mbinguni hakuna namna..

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Bwana akubariki.

Mada Nyinginezo:

Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?

Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu ni wakina nani?

Je! ni halali kutoa cheti kwa wakristo wanaooa?

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

Je unaweza usisamehewe hapa duniani na kule ukasamehewa?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2019/12/07/kiungo-chako-kimoja-kikikukosesha-kikate/