Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?

Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?

Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie katika Ufunuo 19:10 alikuwa ni nani, Je! ni Mwanadamu au Malaika?

JIBU: Tusome…

Ufunuo 19: 10 “ Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”.

Mtu anayetumika kama wewe huyo ni Mjoli wako. Mfanyakazi anayefanya kazi kama ya kwako huyo ni mjoli wako na wewe ni mjoli wake…Hivyo katika Mstari huo hapo juu Yohana alikuwa anataka kumsujudia yule aliyekuwa anazungumza naye,aliyekuwa anamwonyesha maono yale…Lakini akamzuia na kumwambia mimi ni mjoli wako (maana yake ninayafanya kazi kama ya kwako ya utumishi)..na pia wa ndugu zako (yaani wanadamu wenzake ambao ndio sisi tulio na ushuhuda wa Yesu).

Malaika ni wakina nani?

Kwasababu Biblia inasema Malaika ni roho watumikao..wanaotuhudumia sisi(Soma Waebrania 1:3-14)..Kadhalika na sisi wanadamu tunaomtumikia Mungu ni Watumishi wa Mungu vile vile…tunaotumika katika Ufalme wa Mbinguni..Hivyo sisi pamoja na malaika ni Watumishi wa Mungu wa mbinguni…Kwahiyo sisi ni wajoli wa Malaika na Malaika vile vile ni wajoli wetu.

Kwahiyo tukirudi kwenye hilo swali linalouliza.. “aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?”…Jibu lake ni kwamba alikuwa ni MALAIKA. Kwasababu Yohana tangu mwanzo alikuwa haonyeshwi maono yale na mwanadamu yoyote…bali Malaika ambaye naye huyo Malaika aliyapokea maono hayo kutoka kwa Yesu Kristo mwenyewe. Hakuna mwanadamu yoyote aliyehusika hapo kwa namna moja au nyingine..

Ufunuo 1:1 “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma KWA MKONO WA MALAIKA akamwonyesha mtumwa wake Yohana”

Wapo watu wanakosa shabaha katika hilo kudhani kuwa Yule alikuwa ni mtakatifu Fulani aliyekufa zamani au aliyepaa pengine Musa au Eliya, au Nabii Fulani, kwamba ndiye aliyemwambia maneno hayo asimsujudie kwa kuwa yeye ni mjoli wake na wa ndugu zake walio na ushuhuda wa Yesu. Japo ambalo si la kimaandiko..Lakini sasa tunajua kuwa yule hakuwa mwanadamu bali ni Malaika wa mbinguni.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Bwana akubariki.

Maran atha!

Mada Nyinginezo:

UFUNUO: Mlango wa 19

DANIELI: Mlango wa 1

ESTA: Mlango wa 1 & 2

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

ALIKUWAKO NAYE HAYUKO, NAYE YU TAYARI KUPANDA KUTOKA KUZIMU.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments