KUOTA UMEGANDA

by Admin | 13 April 2020 08:46 am04

SWALI: Shalom, nimekuwa na shida usiku nakuwa kama nimeganda siwezi kusogeza mkono au mguu au kuongea lakini akili nakuwa bado ninayo huwa nakemea inachukua muda kidogo naachiwa nashindwa kujua tatizo ni nini naomba nisaidie.


JIBU: Ndoto yoyote ambayo inakuja, na unajikuta katika mazingira ya kupambana na hali Fulani na huku unatumia jina la Yesu, ambapo mwanzoni inaonekana kuleta upinzani Fulani lakini baadaye inakuja kuachia kwa jinsi unavyozidi kuendelea kukemea ni ndoto yenye ujumbe kutoka kwa Mungu..

Wengine wanaota wanashindana na wachawi, na wale wachawi mwanzoni ni kama wanataka kumshinda lakini baadaye anawashinda kwa jina la YESU, wengine wanaota wamekutana na roho za mapepo, halafu kila alipolitaja jina la Yesu sauti, haitoki, lakini kwa jinsi alivyokuwa anaendelea kulitaja mwisho wa siku sauti inatoka na anayashinda.. Mwingine hata sio mapepo bali hali fulani ya udhaifu, kama hiyo ya kwako, unajikuta umeganda huwezi kusogeza kiungo chako hata kimoja, kila unapojaribu unashindwa, unajikuta unahitaji msaada kwa kulitaja jina la Yesu, na unapofanya hivyo mwanzoni ni kama inashindakana lakini baadaye inaachia hali hiyo  inaisha ghafla..

Zote hizo ni ndoto zenye ujumbe mmoja,..Ambao ni Mungu tu anakuonyesha SILAHA pekee ambayo inayoweza kukupa ushindi dhidi ya adui yako shetani, na silaha hiyo tayari umeshaijua ambayo ni jina la YESU. Hivyo ni kuongeza bidii ili uwe na mamlaka kamili juu ya jina hilo kuu.. (Kumbuka mamlaka hayaji kwa kulitamka tu kama ulivyoona kwenye ndoto, bali yanakuja kwa kumwelewa Yesu Kristo katika Neno lake, ndipo kutamka kwako kuwe na nguvu).

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”.

Unaona hakuna lolote litakalokushinda, ikiwa maneno ya Mungu yatakuwa ndani yako kwasababu utakuwa umepewa mamlaka kamili na Kristo mwenyewe ya kushinda mambo yote..

Luka 10:19 “Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru’’.

Hivyo jitahidi kumjua Kristo zaidi, au ongeza  bidii, ili upokee mamlaka hayo kamili..Ndio ujumbe mkuu unaopewa hapo.

Vile vile sababu nyingine ya pembeni, ambayo unapaswa ujue katika ndoto kama hizo za kujikuta umeganda kitandani na huwezi kufanya chochote, ambapo wengine zinakuja katika uhalisia kabisa kana kwamba  sio ndoto, bali ni kitu halisi na wanajiona hawawezi kusogeza kiungo chao chochote kitandani, na anatamani hata mtu amsaidie kusogeza mkono wake  lakini hawezi kumwambia, na wengine wanasema amekufa lakini yeye anajiona bado ..Ni kwamba hapo Mungu anakuonyesha, hali halisi ya jinsi watu wanavyokufa, na  Kwamba yapo maisha baada ya kufa, sio kama wengine wanavyodhani, ukifa huelewi chochote, La, ukifa roho yako inaendelea kuishi inaondolewa katika mwili wako na kupelekwa mahali pengine..(Mhubiri 12)..

Hivyo siku ya kufa, kila mtu atajiona jinsi anavyotoka katika mwili wake na kwenda sehemu nyingine, na ataona pia wanaomzunguka jinsi anavyowaacha!.

Hivyo tunapaswa tujiulize , je! tumejiandaaje huko tuendako? Jibu lipo katika maisha ya kila mmoja jinsi anavyoishi.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Group la whatsapp  Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp


Mada Nyinginezo:

JINSI YA KUSOMA BIBLIA.

KUOTA NYOKA.

JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

WAKATI WA JIONI KUTAKUWAKO NA NURU.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/04/13/kuota-umeganda/