by Admin | 24 April 2021 08:46 pm04
Jibu: Tusome,
Mathayo 5:18 “Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Yodi ni neno lililotumika katika lugha ya Kiswahili cha zamani, lenye maana ya “herufi ndogo”.. kwa lugha ya kiingereza ni “small letter”. Katika sentensi yoyote huwa kunakuwa na herufi kubwa na herufi ndogo, sasa zile ndogo ndio zinazoitwa “yodi”.. Mfano tunaposema neno “Yesu ni Mungu”..Herufi kubwa hapo ni hiyo “Y” na “M” lakini hizo nyingine zote zilizosalia kama “e” “s” “u” “n” “i” “u” ni YODI.
Kwahiyo Bwana Yesu aliposema kwamba hakuna hata “yodi” moja wala nukta itakayoondolewa hata yote yatimie maana yake.. ni kwamba hakuna herufi yoyote (hata ile iliyo ndogo kuliko zote, ‘yodi’) itakayobadilishwa katika maneno ya torati, kwasababu maneno ya Mungu hayabadilii. Ndio maana ukianzia juu kidogo utaona anasema hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza..
Mathayo 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie”.
Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
Pale torati iliposema “usizini”..Bwana Yesu hakuja kulibadilisha hilo andiko, bali alikuja kulitimiliza kwa kusema “mtu amtazamaye mwanamke amekwisha kuzini naye nafsini mwake”. Hapo hajaondoa chochote, bali ameongezea dawa. Torati inaposema “usiue” Bwana Yesu alisema “amwoneaye ndugu yake hasira hana tofauti na muuaji, hivyo itampasa hukumu tu kama muuaji”. Hapo hajaitangua wala kulibadilisha bali ameitimiliza, na sheria nyingine zote za kwenye torati ni hivyo hivyo..
Je wewe bado una chuki kwa ndugu zako au maadui zako?,ukijitumainisha kwamba wewe si muuaji?.. bado unatamani ukijitumainisha kwamba wewe sio mzinzi??, bado unavaa nusu uchi,na suruali ukijitumainisha kwamba wewe si kahaba?? (kasome Mithali 7:10 ujipime kama wewe ni kahaba au la kwa mavazi yako), bado unajichua na kunatazama pornography ukijitumainisha kwamba wewe si mwasherati?, bado ni mshabiki wa mambo ya kidunia kuliko kitu kingine chochote ukijitumainisha kwamba wewe si wa kidunia??.
Kama unafanya mojawapo ya hayo, au yote, wakati wa kumkaribisha Mwokozi ndani ya maisha yako ni huu?..Usingoje kesho wala baadaye, saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubaliwa ndio huu.. wakati wa kukimbilia Kalvari, Bwana akuokoe na kukutua mzigo ndio huu, sio kesho, kwasababu hujui kesho yako itakuwaje, labda leo ndio mwisho wako wa kuishi duniani, au leo ndio siku parapanda ya mwisho itakapolia, jiulize, unyakuo leo ukipita utakuwa wapi??.. Hivyo fanya uamuzi wa kumgeukia Yesu leo kwa kutubu dhambi zako zote kwake, na kwenda kubatizwa katika ubatizo wake wa maji tele (Yohana 3:23), na kwa jina la Yesu Kristo (Matendo 2:38), na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu, atakayekuongoza katika kweli yote ya maandiko.
Maran atha.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Mlima Gerizimu na Ebali ni ipi, na umuhimu wao rohoni ni upi?
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/04/24/yodi-ni-nini-kama-tunavyoisoma-katika-mathayo-518/
Copyright ©2025 unless otherwise noted.