by Devis | 17 June 2022 08:46 pm06
Jibu: Biblia haitupi andiko la moja kwa moja kuwa uchongaji wa ndevu au nywele ni dhambi. Hilo hasaa linategemea na nia, au kiwango , au mtindo. Hapo ndipo yaweza kuwa rahisi kuhukumu kama ni dhambi au la!. Kwamfano mwingine amenyoa kawaida, kisha kwa kumalizia akapenda kuzichonga kwa lengo la kuzifanya ziwe katika mpangilio wake bora lakini hana nia nyingine yoyote, hiyo sio dhambi.
Lakini mwingine anaweka ndevu au nywele zake katika mitindo, fulani mfano tu watu wa kiulimwengu, mfano anachonga pembeni, kisha katikati anaacha kimchirizi kidogo cha nywele (kiduku), utajiuliza huyu mtu nia yake ni nini? Sisi tumeambiwa, Nuru yetu iangaze mbele za watu, ili watakapoona matendo yetu wamtukuze Baba yetu wa mbinguni.. Lakini wewe kama mkristo, unayechonga nywele kwa mitindo hiyo, ni nuru gani unaangaza?
Hali kadhalika tumeambiwa tusiifuatishe namna ya dunia hii (Warumi 12:1).
Hatuna budi kufahamu kuwa miili yetu ni makao ya Mungu, mwenyewe, hivyo lolote tunalolifanya ni lazima tujiulize kwanza mwenye hekalu anapendezwa na huu mtindo ninaomwekea, ikiwa amani ya Kristo ipo ndani yako na una ujasiri wote kumuhubiri Kristo katika hali hiyo fanya, lakini ikiwa hakuna amani, acha mara moja.
1Wakorintho 3:16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je kwa mkristo aliyeokoka, ni dhambi kunyoa ndevu zake?
Kwanini ndugu wanaokaa pamoja wawe kama mafuta ya Haruni?
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/06/17/je-kuchonga-nywele-na-ndevu-ni-dhambi/
Copyright ©2025 Wingu la Mashahidi unless otherwise noted.