SWALI: Je kwa mkristo aliyeokoka, ni dhambi kunyoa ndevu zake kulingana na huu mstari?
Walawi 19:26 “Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi. 27 MSINYOE DENGE PEMBE ZA VICHWANI, WALA MSIHARIBU PEMBE ZA NDEVU ZENU. 28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana. 29 Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu”.
Walawi 19:26 “Msile kitu cho chote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.
27 MSINYOE DENGE PEMBE ZA VICHWANI, WALA MSIHARIBU PEMBE ZA NDEVU ZENU.
28 Msichanje chale yo yote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana.
29 Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu”.
JIBU: Wana wa Israeli wakiwa jangwani Mungu aliwapa maagizo hayo, ya kutokunyoa ndege(para) kwenye pembe za vichwa vyao, na wala wasichonge ndevu (kwa pembeni) wanyoapo.
Sasa Mungu kuwapa maagizo hayo, haikuwa kwasababu wataonekana na mwonekano tofauti, hapana bali mitindo hiyo ilikuwa ni inamaana kubwa Zaidi kwa watu wale, kwani ziliwakilisha ibada za miungu yao ya kipagani na ushirikina. Wakati ule wamisri na waarabu waliokuwa wanaishi majangwani, walikuwa wananyolewa nywele zote za pembeni na kuachwa na KIDUKU cha mvuringo hapo juu, na wengine walikuwa wananyoa para kabisa,(Isaya 15:2, Yeremia 48:37) walifanya hivyo kwa heshima ya miungu yao. Vilevile na kuchongwa kwa pembe za ndevu zao, kwa lengo hilo hilo.
Sasa Ili Mungu kuwatofautisha watu wake na mionekano ya kipagani, akawazuia wasifanye vile kama wao. Mungu alilichagua taifa la Israeli liwe takatifu, lijulikane kama ni taifa la Yehova, sio taifa ambalo watu akilitazama waone desturi za miungu ya kipagani ndani yao. Na ndio maana utaona mpaka “chale” alikataza wasichanjwe, mpaka michoro ya mwilini (Tatoo) wasichore, kwasababu zote hizo zilikuwa ni desturi za wachawi na miungu ya kipagani.
Kama vile wafanyavyo wachina leo hii, utawaona wamenyoa vichwa vyao vyote, na kuacha kifuniko kidogo cha nywele hapo juu, sio kwamba ni fashion hapana, bali ni wanatangaza desturi za miungu yao.
Hata leo hii, Ni ajabu sana kumuona mkristo ananyoa KIDUKU, wala hata hajui asili yake ni nini au anatangaza nini.. Na hata kama hana nia ya kutangaza upagani, lakini pia hajui kuwa Mungu ametuita kujitofautisha na watu wa ulimwenguni, kama alivyofanya kwa waisraeli.
Unaponyoa kiduku, halafu ni mkristo, unatoa nuru gani kwa jamii inayokuzunguka. Ni wazi kuwa unatangaza usanii wa wanamiziki, unapovaa nguo iliyochanika chanika magotini, unatangaza nini?.. Unapofuga rasta, unamtangaza Mungu gani hapo, wewe kama mkristo unatangaza nini..? Kumbuka sisi ni barua tunayosomwa na watu wote.
Pia upo unyoaji wa ndevu wa kisasa ambao unaweza ukawa hauna maana ya ibada ya kipagani, lakini staili ya unyoaji wake zikakutambulisha wewe ni nani, kama utanyoa ndevu kwengine kote halafu hapo katikati unaziacha zirefuke ziwe kama za mbuzi, au unanyoa kisha unaziwekea mitindo mitindo uonekane kama msanii Fulani kwenye tv, wewe kama mkristo unapaswa ujue bado ni rafiki wa dunia. Na sio wa Mungu.
Hivyo kama wewe ni mnyoaji wa viduku, au wa hizo staili ni heri ukaacha, kwasababu Mungu hapendezwi ni mkristo wa namna hiyo.
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.
Warumi 12:1 “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?
Kikuku/vikuku ni nini katika biblia?
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
UFUNUO: Mlango wa 15
Swali: Je Ni sahihi kwa Mkristo kupeleka kesi mahakamani?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 9 (Kitabu cha Ayubu).
Rudi nyumbani
Print this post
Nimependa mafundisho yako
Barikiwa sana mwalimu kwa maarifa haya, binafsi nimukuwa mwathirika wa hili kwa muda mrefu na nilijiona nipo sahihi kabisa likini kwa rehema zake taratibu alianza kuniongoza katika mapenzi yake juu ya hili.Shukrani ni kwake Yeye.