Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)

by Admin | 13 July 2022 08:46 am07

Kuhimidi kibiblia ni kumpa Mungu sifa iliyochanganyikana na heshima na unyenyekevu wa hali ya juu sana,

Neno hili limeonekana  mara nyingi sana katika biblia,

Kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu, ambavyo utakutana na Neno hilo;

Mwanzo 14:19 “Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote”.

Waamuzi 5:3 “Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli”.

Zaburi 31:21 “Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma”.

Zaburi 34: 1 “Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima”.

Warumi 15:10 “Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.

11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.

Ikiwa wewe ni mwanadamu mwenye pumzi huna budi kumuhimidi Mungu muumba wako sikuzote za  maisha yako. Ni lazima ujishushe, upige magoti, na kwa kumaanisha kabisa, umsifu kwa nguvu zako zote, umtukuze kwa wema wake wako, na kuliadhimisha jina lake.

Moja ya mambo ambayo yalimfanya Daudi awe kipenzi cha Mungu, ni tabia yake, ya kumuhimidi Mungu, tena mbele ya makusanyiko ya watu.

Zaburi 26:12 “Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana”.

Bwana atusaidie sote, tuwe na matamanio kama haya.  Kwasababu kama ilivyo chakula chetu sisi ni Neno la Mungu, halikadhalika chakula cha Mungu wetu ni Sifa. Hatuna budi kumlisha kila siku sifa zake, kwa kumuhimidi yeye.

Bwana akubariki.

Je umeokoka? Kama la unafahamu kuwa tunaishi katika vizazi ambacho unyakuo ni wakati wowote?. Tubu dhambi zako mgeukie Mungu, naye atakusaidia. Ikiwa utahitaji msaada ya kumkaribisha Kristo maishani mwako/ kubatizwa, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia?

Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?

Kujazi ni nini? (Mathayo 6:4)

Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

Uchaga ni nini? (Luka 12:24)

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/07/13/kuhimidi-ni-nini/