by Admin | 28 October 2022 08:46 am10
SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani aliposema “nimeaminiwa uwakili”?
1Wakorintho 9:16 “Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! 17 Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili”.
JIBU: Mtume Paulo aliifanya kazi ya Mungu, kana kwamba ni muajiwa/kibarua aliyepewa dhamana ya kusimamia kazi zote alizowekewa chini yake kwa uangalifu, kana kwamba akipoteza chochote au akileta hasara ya jambo lolote atawajibishwa, na boss wake utakapofika muda wa mahesabu.
Tofauti na mtu aliyejitolea tu kazi, kama kusaidia, mtu wa namna hiyo hata akiacha wakati wowote, hawezi kuwajibishwa zaidi sana atapewa shukrani, kwa kutoa mchango wake katika shughuli hiyo, na kupewa viposho.
Ndio maana ya hiyo kauli, “nimeaminiwa uwakili”..kwa lugha nyepesi “nimeamiwa kazi ya mtu mwingine niisimamie kama kijakazi” Na hiyo ndiyo iliyompelekea Mtume Paulo, kusema mimi ni ‘mtumwa na mfungwa’ wa Yesu Kristo (Warumi 1:1,Waefeso 3:1).. Kwasababu hiyo akaitenda kazi ya Mungu kwa uaminifu wote, na kwa umakini wote, hata zaidi ya mitume wengine.
Ni funzo gani tunalipata.
Nasi pia tukiichukulia kazi ya Mungu kama sio jambo la hiari, au la kujitolea tu, bali kama ndio sehemu ya kazi yetu tuliyoajiriwa na Mungu hapa duniani, na kwamba tusipoifanya kwa uaminifu tukaleta hasara, tutatolea hesabu yake siku ya mwisho,..
Yaani tukimtumikia Mungu kama vile tuzitumikiavyo kazi zetu maofisi, bila kuwa na udhuru wowote.
basi tutajifunza kuitenda bila ulegevu Na mwisho wake utakuwa ni kupewa thawabu kubwa na kutukuzwa sana na Bwana Yesu tutakapofika kule mbinguni.
Lakini kama tutajitoa kwa Mungu pale tunapojisikia tu, au tunapokuwa na nafasi, au tunapokumbushwa, au tunapofanikiwa sisi si watumwa au wafungwa wa Yesu Kristo, bali ni watumishi wake tu. Hatujafikia hatua hiyo ya kuitwa watumwa wake.
Bwana atujalie utumishi bora, kama huo, wa kuaminiwa uwakili
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
UTAMBUE UJUMBE WA SAA UNAYOISHI.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/10/28/paulo-alikuwa-na-maana-gani-aliposema-nimeaminiwa-uwakili/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.