by Admin | 21 November 2022 08:46 pm11
Jibu: Kutoka 40:20 “Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku”.
Kiti cha Rehema kilichokuwa juu ya Sanduku la Agano hakikuwa “kiti” kama viti hivi tuvijuavyo, vyenye miguu minne, na vyenye nafasi ya Mtu kuketi.. Bali neno “kiti” kama lilivyotumika hapo limemaanisha “Nafasi ya wazi”.
Kwahiyo juu ya sanduku la Agano hakukuwa na Kitu Fulani mfano wa “Stuli” juu yake, hapana! bali palikuwa na nafasi wazi ambayo ndiyo iliyoitwa “kiti cha rehema”. Nafasi hiyo ilikuwa ipo katikati ya wale Makerubi wawili wa dhahabu ambao walikuwa wanatazamana, na mbawa zao kukutana kwa juu na kuifunika hiyo sehemu ya wazi (yaani kiti cha rehema).
Nafasi hiyo haikuwa kubwa sana, na pia ilikuwa ni sehemu ya mfuniko wa Sanduku zima (maana yake wale Makerubi wawili pamoja na kile kiti cha rehema vilikuwa vimeungana, na kwa pamoja kufanya mfuniko wa sanduku), na ndani ya sanduku kulikuwa na Mana, zile Mbao za mawe zenye amri kumi pamoja na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka. (Tazama picha juu).
Hivyo ulipofika muda wa Upatanisho, Kuhani Mkuu aliingia na damu Ng’ombe na kwenda kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema mara saba, na damu hiyo inakuwa ni upatanisho kwa wana wa Israeli, dhidi ya dhambi zao.
Walawi 16: 14 “Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng’ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba”.
Katika Agano la kale, Israeli walikitazama hicho kiti cha Rehema kama kitovu chao cha kwenda kupata msamaha, kupitia kuhani mkuu wao aliyeteuliwa kwa wakati huo.
Lakini kiti hicho cha rehema kilikuwa na mapungufu yake, kwasababu watu hawakuwa wanapata msamaha wa dhambi, bali dhambi zao zilikuwa zinafunikwa tu!, na kulikuwa na kumbukumbu la dhambi kila mwaka….kwamaana damu za Ng’ombe na Kondoo haziwezi kuondoa dhambi za mtu, vile vile Makuhani wa kibinadamu ambao nao pia wamejaa kasoro hawawezi kuwapatanisha wanadamu na Mungu, kwasababu wao pia ni wakosaji!.. Na pia kiti cha rehema ambacho kipo duniani, kilichotengenezwa na mikono ya wanadamu hakiwezi kufanya utakaso mkamilifu wa dhambi, kwasababu na chenyewe kimetengenezwa na mikono ya watu wenye dhambi..
Hivyo ni lazima kiihitajike kiti kingine cha Rehema kilicho kikamilifu ambacho hakijatengenezwa na mikono ya wanadamu, na vile vile ni lazima ipatikane damu kamilifu ya Mwanadamu asiye na kasoro, na hali kadhalika ni lazima apatikane kuhani Mkuu ambaye hana dhambi..Ndipo UTAKASO na UPATANISHO WA MWANADAMU UWE KAMILI.
Na kiti hicho cha Rehema kipo Mbinguni sasa, na kuhani Mkuu mkamilifu tayari tumepewa, ambaye si mwingine zaidi ya YESU, na damu kamilifu isiyo na kasoro imeshamwagwa kwaajili yetu, na damu hiyo si NYINGINE ZAIDI YA DAMU YA YESU. Hivyo Msamaha mkamilifu unapatikana sasa, na upatanisho mkamilifu unapatikana sasa kupitia Damu ya YESU, kwa kila aaminiye.
Waebrania 9:11 “Lakini Kristo akiisha kuja, ALIYE KUHANI MKUU wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa HEMA ILIYO KUBWA NA KAMILIFU ZAIDI, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu
12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali KWA DAMU YAKE MWENYEWE aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele”.
Je umemwamini Yesu na kuoshwa dhambi zako? Na kupata ukombozi mkamilifu?. Kama Bado unasubiri nini? Kiti cha Rehema kipo wazi sasa, lakini hakitakuwa hivyo siku zote, siku si nyingi baada ya unyakuo kupita mlango wa Neema utafungwa.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.
INJILI NI UWEZA WA MUNGU, UULETAO WOKOVU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2022/11/21/kiti-cha-rehema-kilikuwaje-kutoka-4020/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.