KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.

KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.

Kutubu sio kuomba rehema kwa Mungu!.


Jina la Bwana libarikiwe.

Ipo tofauti kati ya kutubu na kuomba rehema…Wengi tunaomba rehema lakini hatutubu…Ndugu, Rehema bila Toba ni bure!.

Kuomba rehema hakuna tofauti na kuomba msamaha…Unapomwomba Mtu msamaha hapo ni umemwomba rehema…(akurehemu), Lakini Toba haiombwi, toba ni inafanywa na wewe.

Sasa Toba/kutubu ni nini?

Toba maana yake ni KUGEUKA NA KUCHA KILE ULICHOKUWA UNAKIFANYA. Ulikuwa unakwenda mbele ghafla ukaghairi ile njia uliyokuwa unaiendea na kugeuka nyuma na kurudi ulikotoka au kuiendea njia nyingine kutokana labda na sababu fulani ambazo unazijua wewe….sasa hicho kitendo cha kugeuka na kughairi ndicho kinachoitwa Toba. Lakini kuomba msamaha sio kutubu.

Ili kuelewa tofauti Zaidi tofauti ya vitu hivi viwili..tafakari mfano ufuatao.

Mzazi kamwita mwanawe ili amtume mahali, lakini yule mtoto akamfanyie jeuri mzazi wake yule na kumtusi na akaenda kuendelea na michezo…Wakati yupo njiani anaelekea kwenye michezo njiani, dhamiri ikamchoma akagundua amefanya kosa…Hivyo akaghairi safari yake ya kwenda kwenye michezo, akarudi kwa mzazi wake..akampigia magoti akamwambia nisamehe Mama kwa jeuri yangu nimekosa, nipo tayari kwenda kule ulikonituma.

Sasa mtoto huyo pale alipokuwa njiani na kughairi njia yake na kugeuka na kurudi kwa Mama, Hapo ndipo alipotubu…Na hatua ya pili kwenda kumwomba mama yake msamaha kwa jeuri yake ile pale ndipo alipoomba Rehema. Hivyo umeona tofauti ya mambo hayo mawili?…Hauwezi ukasema umeomba rehema na huku hujatubu…Toba inaanza ndipo ndipo kuomba rehema kunafuata.

Ndio mfano ambao Bwana Yesu aliutoa juu ya wale wana wawili..Tusome

Mathayo 21:28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili; akamwendea yule wa kwanza, akasema, Mwanangu, leo nenda kafanye kazi katika shamba la mizabibu.

29 Akajibu akasema, Naenda, Bwana; asiende.

30 Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.

31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili…”

Wakati huu wa matatizo haya yaliyoikumba dunia..sio wakati wa kuomba rehema…ni wakati wa kutubu, maana yake ni wakati wa kuacha dhambi…kughairi mabaya tunayoyafanya…kughairi rushwa tulizokuwa tunakula na tunazoendelea kuzila sasa, ni wakati wa kuacha uasherati kabla ya kumkaribia Mungu wetu kumwomba rehema…ni wakati wa kutupa na kuchoma vimini…niwakati wa kutupa mahereni, mabangili, na kuondoa make-up na kutuacha kuwa asili kama Mungu alivyotuumba, na baada ya hapo ndipo tunamwambia Baba tumeacha sanamu zote hizi tunaomba uturehemu..Ni wakati wa kuwarudishia watu vitu tulivyowarusha au kuwatapeli, ni wakati wa kuwasamehe waliotukosea, ni wakati wa kupatana na ndugu zetu ambao tulikuwa tumewachukia mpaka tukawawekea  vinyongo, Ni wakati wa kuacha kutukana kabisa, ni wakati wa kuacha kuwaseng’enya jirani zetu na kuwatakia shari, Ni wakati wa kuacha ULEVI, na kwenda Disko, ni wakati wa kuacha starehe za kidunia na kumgeukia Mungu..

Tukiyafanya hayo, mbele za Mungu wetu ndio tutakuwa tumetubu..kwasababu tutakuwa tumegeuka na kuziacha njia zetu mbaya..na hivyo akiona Toba yetu hiyo ndipo hata pasipo kutumia nguvu nyingi kuomba rehema..yeye mwenyewe ataturehemu kwasababu ni mwingi wa rehema…Lakini tukienda na lipstick zetu midomoni, mbele zake kumwomba rehema, tukienda na zinaa zetu mbele yake kumwomba aturehemu, tukienda na nguo zetu za nusu uchi mbele zake na kumwomba msamaha…Ni sawa na kijana anayekwenda huku amelewa pombe na huku ana sigara mdomoni mbele za Baba yake na kumwambia Baba naomba unisamehe kwa ulevi wangu. Hapo atakuwa anamdhihaki mzazi wake. Na ndivyo tunavyoonekana mbele za Mungu wetu tunapokwenda kumwomba rehema huku bado hatujadhamiria kuacha dhambi zetu tunazozifanya kwa siri au kwa wazi.

Wakati huu tunayo nafasi ya kuomba rehema kwaajili ya nchi Pamoja na nafsi zetu na ndugu zetu…Ni wakati wa kutanguliza TOBA kwanza kabla ya REHEMA. Na hilo linatosha kabisa kupata rehema bila hata ya sisi kutumia nguvu nyingi…Kama Habari ile ya mwanampotevu..alipoghairi Maisha yake yale na kugeuka kuamua kurudi kwa Baba..hata alipokuwa mbali Baba yake alimwona na kumpokea..hakutumia nguvu nyingi sana Kupata rehema kutoka kwa Baba yake.

Bwana akubariki, kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako..unangoja nini?..Wewe ni shahidi wa nyakati hizi tunazoishi na majira haya..bado makubwa zaidi ya haya unayoyaona yanakuja huko mbeleni kwa wote ambao wapo nje ya Kristo. Hivyo tubu leo na Bwana atakurehemu na kukupa Roho wake Mtakatifu kwasababu anatupenda sana.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

USIISHIE KUTAZAMA JUU, ENDELEA MBELE.

MTINI, WENYE MAJANI.

JE MOYO WAKO NI MNYOFU MBELE ZA MUNGU

JE UNAMTHAMINI BWANA?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Adasa
Adasa
2 years ago

Ninaomba niwe ninatumiwa masomo Kwa barua pepe.

Saimon Raphael Mwansile
Saimon Raphael Mwansile
3 years ago

Be blessed!

Saimon Raphael Mwansile
Saimon Raphael Mwansile
3 years ago

“God bless you servant of God”